NA KAIS MUSSA KAIS.
Ule mjadala ulioanzishwa na mtandao huu bora wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com kuhusu waongozaji wa muziki wa taarab kuweka vipande vya dansi katika nyimbo zao, leo mfalme mzee yusuph nae ametoa maoni yake kama muongozaji na alikuwa na haya ya kuzungumza.
|
MZEE YUSUPH. |
Unajua ndugu mwandishi kuiga katika muziki si vibaya ila inatakiwa utumie akili kugeuza kile unachokiiga ili kiweze kufanya vizuri kwa mashabiki na wadau wanaotuzunguka kwa ujumla, lakini sasa hivi kumezuka mtindo kwa baadhi ya waongozaji wa muziki huu kukopi na kupesti vipande vya dansi kama vilivyo na kuviweka katika muziki wetu wa taarab, hii nasema si sawa kabisa na kwa upande wangu sipo tayari kufanya hivyo hata mara moja.
Ukisikiliza wimbo wangu wa "aliekutwika" unafanana na wimbo wa "evelina" wa Aurus mabelee wa kongo lakini tofauti iliyopo ni kuwa yeye kaimba nami nikageuza nikaupiga kwa kinanda na magitaa kwahiyo mtu kujua ni lazima nimwambie au awe anaujua sana muziki! huu ndio usanii sio kuiga pasipo kuumiza kichwa!. huko nyuma hata akina Mlamali na zanzibar star's na mzee wetu mohamedy elyas walikuwa wanaiga lakini walikuwa wabunifu zaidi nawapongeza!
Nawashauri waongozaji wenzangu wawe wanatumia akili za ziada sana wanapokuwa wanakopi na sio kuhamisha kipande pasipo kukifanyia kazi huu sio muziki tutaendelea kudharauka hata na wasanii wa bongo fleva, tubadilike.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni