Ule msuguano wa wakurugenzi watatu wa bendi za Jahazi modern taarab Mzee yusuph, Amin salmin wa T motto na Omary tego wa coast modern taarab, leo umeingia katika awamu ya pili baada ya mtandao huu bora nchini kufanya mahojiano ya ana kwa ana na Omary tego juu ya kauli ya mzee Yusuph kusema kuwa bendi zao za T motto na coast modern taarab kuitwa magari mabovu!.
OMARY TEGO MKURUGENZI WA COAST MODERN TAARAB. |
Omary tego alianza kwa kusema kuwa mimi nazungumza na mzee yusuph anaongea kwahiyo hapo kuna utofauti mkubwa sana!, naweza kusema kuwa mzee yusuph ananihofia mimi katika kazi, mfano tuliandaliwa onyesho pale travetine pamoja na bendi yake ya jahazi modern taarab, Yeye alimtuma saidi mdoe ili aje aniambie mimi nisipige nyimbo zangu za Chongeni fenicha na Damu nzito sababu alijua nitamgalagaza vibaya!.
Mimi simhofii hata kidogo, yeye ni muoga na ndio maana alikataa kushiriki lile shindano la wapiga vinanda onyesho lililokuwa lifanyike pale Dar live. na amesema kuwa anataka kunitengenezea wimbo, mimi namwambia hana uwezo huo wa kunitungia mimi, kwanza aangalie hizo nyimbo zake je zinafanya vizuri? kaimba chozi la mama imedunda, kaja kaimba mahaba niue imetupwa huko na wadau, na sasa ana hiyo kaning'ang'ania ng'ang'anu nayo sio nyimbo wala nini. mimi namshauri akubali ushindani asapoti vijana wanaokuja sasa kwani sisi itafikia wakati tutaacha hii miziki, roho mbaya sio nzuri.
OMARY TEGO. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni