TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 27 Julai 2015

KIBIBI YAHYA NA SALHA WA HAMMER WAZITOSA BENDI ZAO NA KUJIUNGA NA WAKALIWAO MODERN TARADANCE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Hii sasa ni balaah!, wakaliwao modern taradance au ukipenda waite "Team masauti" kama wanavyojulikana kwa sasa, wameendelea kujidhatiti zaidi baada ya kupata saini za waimbaji wanne wapya kutoka bendi mbalimbali za hapa jijini Dar


           Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo Thabit abdul aliwataja waimbaji hao na bendi walizotokea kuwa ni Kibibi yahya ambae ametokea bendi ya maja's modern taarab, Salha wa hammer ambae ametokea bendi ya five star's modern taarab, Asya hassan "mjusi" ambae ametokea East african melody na Hafidh faith ambae pia ni MC wa bendi huyu anatokea East african melody pia.

KIBIBI YAHYA MUIMBAJI MPYA WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE.

       Pia nipo katika mipango ya kuongeza wapigaji wa vyombo maana kwa waimbaji naona risti imetimia nina waimbaji wazuri kuliko bendi yoyote ile kwa sasa!. Nawaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi wa albam ya "siioni thamani ya pendo" pale Dar live kwani kuna mambo mazuri nimeyaandaa kwa ajili yao, naamini watafurahi sana siku hiyo!, hii si ya kukosa kabisa!. Wakati huo huo mkurugenzi wa wakaliwao thabit abdul amemchagua Kibibi yahya kuwa ndio "matron" wa bendi hiyo ili awaongoze wanawake wenzake katika bendi.


       Zifuatazo ni picha za waimbaji wapya walivyokuwa katika mazoezi siku ya leo:-

SALHA WA HAMMER MUIMBAJI MPYA WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE.
ASYA HASSAN "MJUSI" MUIMBAJI MPYA WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE.
HAFIDH FAITH "MC" WA WAKALIWAO BENDI, ANATOKEA EAST AFRICAN MELODY

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni