Bendi ya wakaliwao modern taradance ambayo inatarajia kufanya uzinduzi wa albam yao mpya ya pili inayokwenda kwa jina la "siioni thamani ya pendo!" imeendelea na mazoezi ya maandalizi ya show hiyo ambayo inatarajia kufanyika mbagala jijini Dar katika ukumbi wa Dar live siku ya jumamosi tarehe 1/8/2015.
Katika show hiyo ambayo imekuwa gumzo kwa sasa katika jiji la Dar, wakaliwao wanatarajiwa kusindikizwa na bendi za Jahazi modern taarab, Ogopa kopa classic bendi, Juma nature, msagasumu, Dogo jacky simela na wataalam wa kisingeli Man fongo na Sholo bomba!. zifuatazo ni baadhi ya picha wakati wakaliwao wakiwa katika mazoezi ya nguvu siku ya leo!.
THABIT ABDUL AKIWA NA OTILIA KATIKA MAZOEZI YA LEO. |
JUMA MKIMA AKIKIPULIZA KINANDA KWA RAHA ZAKE!. |
HAPA ZOEZI KWA KWENDA MBELE...HATAREEEE!. |
MAZOEZI YANAENDELEA HAPA. |
JUMANNE ULAYA NAE ALIKUWEPO...ITAKUWA BALAAH SIKU YA UZINDUZI. |
THABITI ABDUL AKIONYESHA UMAHIRI WAKUSEREBUKA!. |
MKOMBOZI KAZINI...TAREHE 1/8/2015 SIO SIKU YA KUKOSA!. |
OTILIA NA THABIT ABDUL WAKIONGOZA MAZOEZI YA LEO. |
ANAITWA AISHA OTHMAN VUVUZELA AKIWA MAZOEZINI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni