...Wakielekea
makaburini.
Banza
alianza muziki miaka 25 iliyopita, mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya
msingi, akiimba hip hop, na wazazi wake walipoweka pingamizi baada ya kuona
muziki huo kuwa wa kihuni akahamia kuwa mcheza show za dansi kwenye maharusi.
Fedha za
show hizo alizitumia kusomea masuala ya muziki na kumaliza kwenye Chuo cha
Utamaduni cha Korea 1991.
Baada ya
kuhitimu cheti alianza kuimba katika bendi mbalimbali ikiwamo The Heart
Strings, Twiga Band, Achigo Band (kama mpiga ngoma), Afri-Swazi lakini alipata
umaarufu baada ya kujiunga na The Africa Stars 'Twanga Pepeta'.
Banza Stone
amewahi kutamba na nyimbo kadhaa zikiwamo 'Mtaji wa Maskini', 'Kumekucha',
'Elimu ya Mjinga', 'Angurumapo Simba Mcheza Nani' na 'Falsafa ya Maisha.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni