TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 28 Julai 2015

WAKALIWAO MODERN TARADANCE, FATMA SHOBO, PRINCE AMIGO NA DOGO JACKY KUFANYA SHOW YA NGUVU JM HOTEL MANZESE IJUMAA HII.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Bendi inayokuja kwa kasi ya ajabu kwa sasa jijini dar na tanzania kwa ujumla wakaliwao modern taradance au ukipenda waite "team masauti" kama wanavyotambulika kwa mashabiki wake, wakiwa na baadhi ya wasanii wa jahazi modern taarab kama Fatma shobo na Prince amigo bila kumsahau dogo jacky simela mtoto wa jagwa musica wanatarajia kufanya onyesho la nguvu katika ukumbi wa JM HOTEL uliopo manzese jijini dar siku ya ijumaa tarehe 31/7/2015.


WAKALIWAO MORDEN TARADANCE.

        Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema show hiyo itakuwa nzuri kupita kiasi sababu wasanii wake wamepania kuwafunika wasanii kutoka jahazi modern taarab ambao wamekuwa wakitamba sana katika vyombo vya habari kwa muda mrefu sana!, unajua mimi nina kikosi kazi a.k.a. team masauti wanauwezo mkubwa sana wakumsambaratisha yeyote yule kwahiyo nawaomba wapenzi wajitokeze kwa wingi sana siku hiyo ya ijumaa kwani nafsi zao zitaburudika kwa tulicho waandalia alimaliza kwa kusema.


     Bendi hii ya wakaliwao modern taradance itakuwa ikifanya show zake katika ukumbi huo kila siku ya ijumaa kwahiyo wadau na wapenzi wa maeneo ya manzese na vitongoji vyake waje kupata raha za wakaliwao modern taradance a.k.a, team masauti.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni