Bendi za muziki wa taarab nchini tanzania zimeungana kwa pamoja na kutengeneza wimbo mpya wa kuhamasisha jamii ya kitanzania kushiriki kwa amani na utulivu katika zoezi zima la upigaji wa kura ifikapo october 25/2015.
![]() |
| BAADHI YA WASANII WAKIWA MAZOEZINI. |
Wimbo huo uliopewa tittle ya "Tupige kura kwa amani" umetungwa nae mtunzi mahiri El-khatib Job na kutiwa sauti na madirector thabit abdul, Ally J na Omary tego. Akizungumza na mtandao huu makini kabisa msimamizi mkuu wa zoezi hili mzee mbizo alisema nia na madhumuni ya kukusanyika kwa pamoja ni kuihamasisha jamii kushiriki vyema klatika mchakato huu wa upigaji wa kura kwa amani na utulivu mkubwa, na tumeamua kuwakutanisha waimbaji na wapigaji toka bendi mbalimbali hapa nchini ili kuonyesha ule ushirikiano wetu uliopo katika sanaa!.
![]() |
| MASHAIRI YAKIWA MIKONONI, MAZOEZI YANAENDELEA. |


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni