TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 3 Oktoba 2015

PATA HISTORIA YA SHAIBU BESI, MUME HALALI WA MWAMVITA SHAIBU, ALIANZAJE MUZIKI?.

NA KAIS MUSSA KAIS
   +255657036328

             Jina la shaibu maulidi linaweza kuwa gumu kulitambua haraka kulingana na a.k.a. anayoitumia katika tasnia hii ya muziki wa taarab, lakini si mwingine muite shaibu besi mume halali kabisa wa mwamvita shaibu muimbaji ambae amepitia bendi kadhaa na wimbo anaoendelea kutamba nao ni mwenye hila habebeki alioimbia five stars modern taarab.


         Shaibu maulid au ukipenda muite shaibu besi nilifanikiwa kufanya nae mahojiano pale maeneo ya kapakabana mwananyamala A, na kwanza nilitaka kujua historia yake japo kiufupi tu nae alikuwa na haya ya kusema:- Jina langu kamili naitwa shaibu maulidi ila kutokana na chombo ninachopiga katika muziki huu kuwa ni gitaa la besi basi wapenzi wakaamua kunipachika jina la shaibu besi, nimesoma shule ya msingi makurumla pale magomeni kuanzia mwaka 1985 mpaka 1991 nikamaliza la saba, O level nimesoma meta secondary school nikamaliza 1995.


      Baadae nilirudi dar nikasomea ufundi makenika pale mgulani kwa muda wa miaka miwili 1998 mpaka 1999, nilipotoka hapo nikajiunga na chuo cha N.I.T. ubungo jijini dar kusomea udereva kwa muda wa miezi mitatu, hiyo ndio historia yangu nje ya muziki.


                                                             "MAISHA YA MUZIKI".

       Chanzo kabisa cha mimi kuingia katika muziki ni pale nilipokuwa katibu uhamasishaji wa C.C.M. tawi la kagera kisiwani nakumbuka ilikuwa mwaka 1999 mwishoni, tulianzisha kikundi cha uhamasishaji kilichokuwa kikiitwa "DAR ONE THEATRE" tulikuwa tunajishughulisha na ngoma za asili, kwaya, mazingaombwe na maigizo. Nilipoachana na kikundi hicho nikahamia kikundi cha T.M.T. tandale modern theatre au mbeleko kilichopo tandale jijini dar, hapo ndipo nilipoanza kujifundisha ala za muziki hususani hizi zinazotumia umeme, nikachagua gitaa la besi, drums na tumba lakini mpaka sasa nimekuwa mpiga besi mzuri kuliko hivyo vingine ijapokuwa naweza vyote.nakumbuka pale niliwahi kutunga wimbo wa kuhamasisha jamii kuipenda timu yetu ya taifa, taifa star's na ukashinda nafasi ya pili ndani ya cloud's fm redio tukapewa zawadi ya shilingi milioni moja taslimu wimbo uliitwa "Taifa star's kanyaga twende".


     Baadae nilihamia bendi ya lunch time ya manzese nikiwa ni miongoni mwa waanzilishi wa bendi hiyo mwaka 2010, hapo tulikuja kutofautiana baada ya mwenzetu mmoja kutusaliti makubaliano tuliyoadhimia kwa pamoja kama bendi na kwenda kusema kwa mkurugenzi, ndipo tulipojiondoa katika bendi hiyo zaidi ya wasanii sita na kuelekea bendi ya G5 modern taarab chini ya mkurugenzi Hamisi slim na hapo nipo mpaka sasa ninapozungumza. nashukuru maisha yanakwenda na katika ndoa yangu na mke wangu Mwamvita shaibu tumefanikiwa kupata mtoto mmoja ambae anaitwa Husna shaibu mwenye umri wa miaka 8.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni