NA KAIS MUSSA KAIS.
Muimbaji asya mariam "utamu" wa bendi ya wakaliwao modern taradance amerejea rasmi kikosini jana tarehe 25/9/2015 katika show ya kapakabana mwananyamala A jijini dar.
|
ASYA MARIAM |
Akizungumza na mtandao huu Asya mariam alisema kuwa nimerejea rasmi ndani ya wakaliwao modern taradance baada ya kumaliza tofauti zangu na uongozi!. unajua siku zote mnapokuwa mnaishi basi kasoro ndogo ndogo hazikosekani, ila nashukuru tumemaliza na sasa nipo ndani ya bendi yangu ya wakaliwao modern taradance kama kawaida, nawaomba wapenzi wangu wajitokeze kwa wingi leo ndani ya ukumbi wa center gill zamani flamingo wanione na nitawaimbia sioni thamani ya pendo, fungu la kukosa. sambamba na najuta kupenda.
Ikumbukwe kuwa Asya mariam alitofautiana na uongozi wa bendi ya wakaliwao modern taradance hali iliyopelekea kutohudhulia maonyesho kadhaa ya bendi hiyo na maneno mengi yakasemwa kuwa anaenda mashauzi classic na wengine wakisema kuwa anaenda jahazi modern taarab, lakini mwisho wa siku asya mariam amekomesha uvumi huo na kuamua kurudi ndani ya wakaliwao modern taradance!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni