TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 5 Oktoba 2015

WAKALIWAO MODERN TARADANCE KUSHIRIKI TAMASHA LA COAST NIGHT 2015 NAIROBI KENYA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                   Bendi ya wakaliwao modern taradance ya jijini dar baada ya sintofahamu iliyotokea mwaka jana juu ya wao kutoshiriki tamasha la coast night, mwaka huu mambo yameenda vyema kutokana na ubora wa kazi zao na kamati imeamua kuwa huu ni mwaka wa wakaliwao!.


WAIMBAJI WAKALIWAO MODERN TARADANCE.

          Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba mratibu wa tamasha hilo kwa upande wa tanzania bwana Emmanuel kalugira alisema kuwa wakaliwao modern taradance ni bendi bora na kwa kipindi hiki nchini kenya kona zote maneno ni juu ya ubora wao, redio na vituo mbalimbali vya televisheni zimekuwa zikicheza nyimbo za bendi hii, ubora wa kazi za wakaliwao ndio kigezo kikubwa kilichotumika katika kufikia muafaka wa sisi kama kamati kuichagua bendi hii.


DANCER'S WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE WAKIWA KAZINI.

              Mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema kuwa anawaomba wadau na mashabiki wa wakaliwao nchini kenya kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo kwani kikosi kizima cha wakaliwao modern taradance kitakuja na kitakonga nyoyo za wakazi wa nairobi na vitongoji vyake, tamasaha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 6/11/2015 siku ya ijumaa.


           

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni