NA KAIS MUSSA KAIS
Wakati muziki wa Taarab umekuwa na mafanikio makubwa ya
kutumbuiza katika nchi mbali mbali kama vile, India mnamo mwaka 1928
mwimbaji
maarufu Siti Bint Saad alifanya maonyesho na kurekodi baadhi ya
nyimbo, Bi Kidude akiwa pamoja na mpiga ala Mohamed Issa Matona na
wasanii
wengine wengi walizunguka nchi mbali mbali za ulaya kwa ajili ya
kutumbuiza na kuueneza muziki wa taarab asilia, hii ilitakuwa ni mara ya
kwanza kwa taarab kutengeneza njia yake ndani ya bara la Afrika,
kama kusini-magharibi katika nchi ya Zimbabwe.
Ndani ya Afrika kumekuwa na mtiririko wa muziki wenye vionjo na
wenye kueneza mila za muziki zilizomo ndani ya Afrika. Mifano ya hii ni
kuenea
kwa mila ya muziki wa upinde ambao ulisafirishwa kutokana na
uhamiaji wa wangoni mnamo miaka mia moja iliyopita, mila hii iliyotokea
katika pwani
ya Afrika Kusini na kupita kaskazini mwa Malawi na kusini mwa
Tanzania, aina hii ya uimbaji hupatikana katika mila za watu wafupi
waliopo nchini
Kongo na kuenea kusini kupitia sehemu ya Afrika ya Kati na kwenda
moja kwa moja Cape, na hata pia ndani ya Tanzania kabila la Maasai
huimba sana
vionjo vya muziki wa kabila la wagogo.
Wakati uhamiaji wa muziki wa kusini - mashariki uliofanyika miaka
mingi iliyopita, kumekuwa na usawa kidogo wa uhamiaji wa muziki wa
mashariki - magharibi.
Na ndio maana Ziara ya kihistoria ya kikundi cha Taarab-Kidumbak
kutoka chuo cha muziki DCMA - Zanzibar, kilifanya maonyesho kuanzia
Aprili 28 hadi Mei 3,
ni muhimu sana.
Wakati muziki wa Zanzibar umeathirika sana na muziki wa Wareno
kuanzia karne ya 1500 mpaka 1700, mila za Kiarabu kuanzia karne ya 1700
mpaka 1900 na mila za
Ulaya / Marekani (Ujerumani na Uingereza na Umoja wa Mataifa)
tangu mwaka 1900, muziki wa Zanzibar ulikuwa na nafasi ndogo ya
kushawishi desturi za muziki mwingine.
Isipokuwa mila ya muziki kutoka katika Visiwa vya Comoro
vilivyopo kusini mwa Bahari ya Hindi ambayo imekuwa vionjo vyake
vimefanana sana na taarab na miziki ya aina
nyingine kutokea Zanzibar... na baadhi ya mila za muziki wa
Kihindi / Kiajemi kutoka Zanzibar na kuenea katika maeneo ya kaskazini
mwa Uganda.
Alexander MacKay (1848-1890), mmishonari aliyeishi miaka mingi
nchini Uganda, mnamo mwaka 1879 alipendekeza kuwa ngoma na matarumbeta
aliyoona na kusikia katika Buganda
yalikuja kutokea Zanzibar na maeneo mengine katika pwani ya nchi
ya Buganda. Wachsmann (1971) pia alisema kwamba chifu wa Buganda, chifu
Muteesa (Chifu kuanzia 1856 - 1884),
"Kuajiri mkufunzi mwenye ujuzi, ambaye aliyewahi kufanya kazi kwa
Sultani wa Zanzibar kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana katika muziki
wa kupiga ngoma".
Sasa, muziki wa Taarab wa Zanzibar, wenye vionjo vya muziki wa
café ya Misri mnamo miaka 150 iliyopita, ambapo walielekea Zimbabwe kwa
ajili ya maonyesho maalumu katika Tamasha
la kimataifa la sanaa Harare (HIFA).Ubora wa elimu yetu, hii
ilikuwa ni mara ya kwanza kwa tamaduni ya muziki wa taarab na kidumbak
kutoka Zanzibar kutumbuiza mbali na magharibi
ya pwani ya Afrika Mashariki. Wanamuziki 10 kutoka DCMA walifanya
safari hii ya kihistoria na walifanya maonyesho manne (4) katika mji wa
Harare, maonyesho makubwa mawili (2),
kufanya maonyesho katika mitaa ya mji Harare na kufanya warsha za
taarab, kupiga ngoma na kuimba katika mashule.
Ziara hii ya kihistoria ilikuwa ni kumbukumbu na ni dhamira ya
chuo cha muziki cha nchi za jahazi (DCMA) kwamba ziara hii iliwezesha
wananchi wengi zaidi kutoka Zimbabwe na kwingineko
kujifunza zaidi kuhusu utengenezaji, mafunzo ya muziki kutoka
DCMA na kukua kwa tamaduni za muziki wa taarab - kidumbaki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni