TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 5 Novemba 2015

ENRICO FIGUEIREDO PRODUCER BORA WA TAARAB ANAE ZINYANYASA TUZO ZA KILI KILA MWAKA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Anaitwa Enrico figueiredo almaarufu enrico wa sound crafter's huyu ni mwanamuziki mkongwe wa zamani, ameanza muziki tokea mwaka 1976 na alianza kujifunza box gita na baada ya miaka mitatu ndio akaanza kupanda jukwaani rasmi.

ENRICO FIGUEIRO PRODUCER MKUU SOUND CRAFTER'S STUDIO.


         Enrico ameshatumbuiza hoteli nyingi sana hapa nchini tanzania kama vile bahari beach, new africa hotel, kempisk, sheraton hotel pamoja na hotel nyingi za kitalii zilizopo huko mkoani arusha, amesafiri nchi mbalimbali za ulaya akiwa na bendi ya In africa na alikuwa mpiga gitaa la solo mzuri tu, baadae alipopata vyombo vya studio ilibidi ajigawe sasa.Na mwaka 1998 aliamua kujikita zaidi katika masuala ya studio na vile vile enrico ni muasisi wa kurekodi muziki wa rap hapa tanzania kabla hii miziki ya kuimbaimba bongo freva haijaanza, wasanii wengi sana amewatengenezea nyimbo zao za hip hop kama juma nature, zay b, solo thang, chid benzi, sister p na wengineo wengi hawakumbuki wote kwa sasa.


TREZZ MAVOKO PRODUCER SOUND CRAFTER'S STUDIO.

            Kuna muda alienda mwanza akafungua tawi la studio kule na alikaa kama miezi minane akaamua kurudi tena dar, mwaka 2001 alikwenda kusomea jinsi ya kurekodi kwa kompyuta sababu zamani kulikuwa wanarekodi kwa mtindo wa anarogy spou!. aliporudi akaanza kurekodi miziki tofauti ya dansi, kwaya, taarab na hata bongo freva, enrico ni producer wa aina zote za miziki ingawa kwa sasa soko la muziki wa taarab ndio inaonekana ndio yupo sana ila ana uwezo wa kurekodi miziki yote.


ENRICO FIGUEIREDO AKIWA KATIKA UBORA WAKE.

            Anashukuru Ameshafanya kazi na bendi zote za taarab zilizo juu kwa sasa ambazo unazifahamu wewe, na hata bendi ndogondogo pamoja na msanii mmoja mmoja amekuwa akiwafanyia kazi zao kwa ubora wa hali ya juu sana!, siri kubwa ya enrico kufanya vizuri katika muziki huu ni umakini wake katika usimamizi wa kazi zake. mpaka sasa ameshapata tuzo tatu za mtayarishaji bora wa muziki wa taarab nchini kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2013, 2014, 2015 na anaamini mwaka ujao panapo majaaliwa na uhai basi atachukuwa tena kwani ana kazi nyingi sana amezifanya na bendi mbalimbali. msanii ambae anamkubali sana akiwa studioni kwake anarekodi na huwa hapati nae shida ni thabit abdul, huyu jamaa ana kipaji cha hali ya juu ukweli lazima niseme nampongeza sana, vile vile nimekuwa nikichukia msanii anakuja studio kurekodi alafu hata kuifuata beat tu hajui! hili ni tatizo ambalo limenifanya kuwarudisha wasanii wengi tu wakaendelee kujifunza zaidi alimaliza kwa kusema Enrico.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni