TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 15 Novemba 2015

HAUVUMI LAKINI UMO YA ALLY STAR, INAKUKUMBUSHA WAPI?...PATA MASHAIRI YAKE HAPA!.

 Na pambe za taarab
 
 
       "HAUVUMI LAKINI UMO".


ALLY STAR- SHARO BABU!.

KIITIKIO:-


Ama kweli mlezi wako alokulea, Kala hasara

Ama kweli mwalimu wako alokufundisha, Kala hasara

Ama kweli mzito wako alokulea, Una mambo

Ama kweli mchumba wako ulompata, Kala hasara


Mdogo wa kimo una mambo wewe, una mambo wewe, una mambo


Nimeshaamini chochote kizuri hakikosi kasoro

Mama mkata umoja kala hasara huyo

Mtega uchumi kumbe nawe umo

Japo hauvumi kumbe nawe umo

Huko mitaani umepewa jina waitwa mama huruma we


Sikutegemea wala sikudhani kama una mambo


Wala hufanani na jambo la mtoto, una mambo wewe


Kila uonacho, Wakitolea macho wataka kukichukua

Japo siyo chako, Wakitolea macho wataka kukichukua 

 

"UIMBAJI"


1. Nilidhani mimi chanda Na wewe ni pete yangu

Nikawa ninakupenda Kukuona u mwenzangu

Kumbe nimefuga donda Lilowashinda wenzangu 

Ikawa wagawa tenda Hata kwa rafiki zangu

Ikawa wagawa tenda Hata kwa wadogo zangu

Toka bibi fanya nenda Bora niishi kivyangu

Mimi sili vya kuvunda Hili ni zindiko langu

Wewe si mtu ni sanda Na hofu uhai wangu



2. Si kama nakutania Nakueleza bayana

Kwa kweli sikudhania Kama huna maana

Kumbe wewe kisinia Kote unajulikana

Umekuwa zabania Kugonganisha mabwana

Wewe siwakutania Wengi wanapongezana

Wanavyokugombania Kama mpira wa kona

Umegeuka gunia Kubeba kila aina 


3. Mambo yako yanatanda Yazagaa kama wingu

Hupumziki kuranda Kutwa kucha wanguwangu

Unachokijua kwenda Huoni hata uchungu

Mgongo umekupinda Kwa kutaka vya uvungu

Pepo aliekupanda Hapungwi hata kwa nyungu

Nakuambia utakonda Huwezi ulimwengu

Umekuwa paka nunda Wa kunusanusa vyungu


4. Duka lako la asali Sasa linanuka shombo

Waja wamekutapeli Usiyepitwa na jambo

Hivi sasa huna dili Yanakuendea kombo

Ukipewa bia mbili Umekwisha huna nyimbo

Wajanja wenye akili Wanakuuza kimombo

Hujui lile na hili Kazi kufuata mkumbo

Umegeuka egoli, Hupigwi la mgambo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni