TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 10 Novemba 2015

LEO HII UMETIMIZA MWAKA WA PILI TANGIA UTUTOKE NYAWANA FUNDIKIRA, MUNGU AKUONDOSHEE ADHABU ZA KABURI.

NA KAIS MUSSA KAIS.
       0657 - 036328

            Ni siku ngumu sana kwangu miongoni mwa siku nitakazo endelea kuzikumbuka daima katika maisha yangu hapa duniani, tarehe 11/11, uliniacha nyawana isale fundikira nikiwa siamini kile kilichopo machoni mwangu.

MAREHEMU NYAWANA ISALE FUNDIKIRA.

               Nilikuita haukuitika tena, nilijitahidi kukutingisha pia sikupata jibu lolote lile, ndipo kwa hofu na woga nilitoka kwenda kuita wazee ambao wana ufahamu mkubwa walipofika nakukuona waliniambia nijikaze kwani mimi ni mtoto wakiume...haupo tena duniani mke wangu umeiaga dunia!.ni taswira ambayo huwa sipendi kuikumbuka mara kwa mara kwani inaniumiza sana!.nikisema sana nitakuwa namkosea muumba wetu kwani kila kilichopo duniani na kikapewa pumzi na uhai basi kitakufa pia.

        Wewe umetangulia nyawana wangu lakini sisi pia tupo njiani wakati wetu ukifika tutaiaga dunia pia, kikubwa ambacho nimepanga kufanya leo ni dua kwa ajili yako ili mwenyezi mungu akufanyie wepesi katika adhabu zake, watoto wako wapenzi said na Queen wanakukumbuka sana na tupo karibu sana kwa mambo mengi msingi imara ulioujenga kwao juu yangu wameendelea kuwa nao na wananikumbuka kama baba yao. Nina mengi ya kuandika nyawana wangu lakini nahisi nitamkosea mungu na kukosa radhi zake. mimi mumeo kais mussa kais nakukumbuka sana na nakumbuka kwa  mengi mazuri tuliyoyafanya na hata baadhi ya ndoto zetu ambazo tulikuwa tumezipanga! Eeeh! mwenyezimungu mpumzishe kwa amani nyawana wangu milele daima...Amin!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni