TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 9 Novemba 2015

NAJUTA KUPENDA YA ASIA UTAMU IMEFUTWA RASMI LEO NA KUREKODIWA UPYA NDANI YA SOUND CRAFTER'S.

NA KAIS MUSSA KAIS.


               Ule wimbo uliozua gumzo na mijadala mbalimbali inayoendelea mitandaoni kwa wadau kulumbana "najuta kupenda" umefutwa rasmi leo na kurekodiwa upya chini yake muimbaji "Aisha mtamu kabisa" ndani ya studio za sound crafter's temeke jijini dar.

AISHA MTAMU KABISA-AKIIMBA KWA HISIA KALI.


            Wimbo huo ambao unatarajiwa kuanza kuchezwa redioni kuanzia jumapili ya wiki hii umebadilishwa baadhi ya miziki na hata uimbaji kiasi, unajua huyu Aisha mtamu kabisa ana radha flani "amazing" kwahiyo naamini wapenzi na wadau wataupokea wimbo huu kwa bashasha kubwa kwani ameutendea haki alisikika director msaidizi wa studio hiyo Drezz mavoko akizungumza.

DIRECTOR THABIT ABDUL AKIPIGA KINANDA UPYA KATIKA WIMBO HUO!.


       Nae mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul amesisitiza kuwa pindi itakapopelekwa "najuta kupenda" redioni basi nitazipiga stop redio zote kuacha kabisa kucheza wimbo wa najuta kupenda ulioimbwa na asia utamu! badala yake nataka huu ulioimbwa sasa na Aisha mtamu kabisa ndio upewe air time na wala si vinginevyo
!. nawaomba wapenzi wajiandae kusikia ujio mpya wa Aisha mtamu kabisa akifanya yake ndani ya wakaliwao modern taradance alimaliza kwa kusema!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni