TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 1 Novemba 2015

OMARY TEGO:- VIONGOZI WA BENDI ZA TAARAB TUWE NA VIKAO VYA MARA KWA MARA ILI KUUNUSURU MUZIKI WETU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                  Omary tego mkurugenzi wa coast modern taarab ametoa rai yake kwa viongozi wote wa bendi za muziki huu wa taarab nchini kujenga taratibu za kukutana mara kwa mara na kufanya vikao ili kujadiliana juu ya mustakabali au mwenendo wa muziki huu hapa nchini.

 

                 Aliyasema hayo wakati alipopiga simu katika chumba chetu cha habari ili kutaka kujua ni nini haswa nia na madhumuni ya kuanzishwa kwa kundi la wazawa classic modern taarab na thabit abdul, aliposhibishwa kwa hoja na maneno ya msingi ndipo aliposhauri kutengwe siku maalum kama mwisho wa mwezi au katikati watu wa taarab wakutane katika kuyajenga yanayo wahusu.

OMARY TEGO-MKURUGENZI WA COAST MODERN TAARAB.

 

              Kwa sasa tumekuwa hatuna ukaribu hata wakiushauri jambo linalopelekea kujenga matabaka miongoni mwetu hii ni hatari kwa maendeleo ya muziki huu wa taarab nchini. Unajua ndugu mwandishi kwa sasa taarab inapoteza uhalisia wake na chanzo kikubwa ni sisi viongozi tukisingizia eti tunakwenda kulingana na soko la mahitaji ya muziki, hii sio kweli tunapotea na mwishowe taarab itakosa thamani!, hebu jumatatu moja au jumanne nenda pale east african melody lango la jiji magomeni au max bar ilala kaangalie umati unaoingia mule, na melody hawajarekodi siku nyingi sana ila ubora wa nyimbo zao za zamani ndio chachu ya kuendelea kupendwa na mashabiki wao!, hizi taradance kiukweli nyimbo zake hazidumu katika soko, tunapotea viongozi wenzangu hebu turudi nyuma bado hatujachelewa. Laiti kama tungekuwa tunakutana mara kwa mara basi naamini tungekuwa tunakwenda sawa na kwa malengo, naomba wasininukuu vibaya huu ni mtazamo tu viongozi wenzangu! naomba itengwe siku tukutane kwa pamoja jamani alimaliza kwa kusema!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni