TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 2 Novemba 2015

WAKALIWAO MODERN TARADANCE KUWA NA SHOW TATU KALI NDANI YA WIKI HII.

NA KAIS MUSSA KAIS.


              Baada ya likizo ya takribani wiki mbili waliyopewa wasanii wa wakaliwao modern taradance ili kupisha uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani ambao ulifanyika nchi nzima tarehe 25/10/2015, bendi yako uipendayo ya wakaliwao inaendelea na maonyesho yake kama kawaida.


TEAM WAKALIWAO MODERN TARADANCE.

            Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema kwamba sasa kazi moja tu! kuwapa burudani mashabiki wao ambao walikuwa wamewakosa kwa kipindi hicho chote, alizitaja show zitakazo fanyika wiki hii kuwa ni tatu na zinaanza siku ya alhamisi kwa kupiga katika ukumbi wa woodland manzese darajani, siku ya ijumaa burudani itahamia c.c. club ukumbi uliopo maeneo ya msasani karibu na hospitali ya C.C.B.R.T. siku ya jumamosi wakaliwao watakuwa maeneo ya kimara stop over wakimalizia week-end, aliwaomba wadau na mashabiki kujitokeza kwa wingi katika show zao kwani pamoja na burudani lakini T-shirt mpya za wakaliwao modern taradance zitauzwa ukumbini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni