TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 3 Novemba 2015

NAJUTA KUPENDA YA ASIA UTAMU KUREKODIWA TENA UPYA NA AISHA MTAMU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                Ule wimbo unaowaliza wapenzi wengi sana, haswa mashabiki wa muziki wa taarab nchini "najuta kupenda" ambao hapo kabla uliimbwa nae Asia utamu akiwa na kundi zima la wakaliwao modern taradance kwa sasa utarudiwa tena kurekodiwa upya studio na mwana dada mwenye sauti tamu na laini aitwae Aisha mtamu.

        Kwa mujibu ya maelezo ya mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul "mkombozi" alisema kuwa nimeamua kuurudia upya wimbo huu na kuongeza baadhi ya vionjo vya kuunogesha zaidi na kwa sasa utarekodiwa na Aisha mtamu msichana mdogo lakini mwenye kipaji cha hali ya juu sana, najua wadau watakuwa na maswali mengi sana kwanini nimeamua kuiondoa na kuifuta kabisa sauti ya Asia utamu, sababu kubwa ni kuwa sioni sababu ya kuendelea kumbembeleza Asia utamu arudi kazini, ameonyesha utovu wa nidhamu kwa uongozi mzima wa wakaliwao modern taradance kwa kujiamulia kukaa nyumbani wakati tayari alisha samehewa na kuambiwa arudi kazini.

AISHA MTAMU AKIIMBA-NAJUTA KUPENDA.

            Unajua Asia utamu tulishazungumza nae yakawa yameisha, lakini aliposamehewa hivyo na uongozi akaja kazini siku mbili  tu, baada ya hapo hakuja tena!, lakini wakati huo huo alikuwa akionekana katika show za bendi zingine akiimba na kuitosa kabisa wakaliwao modern taradance ikiendelea kufanya show pasipo yeye kuwepo. sasa mimi kama mkurugenzi wa bendi hii nasema kwamba wimbo wa najuta kupenda ulioimbwa na Asia utamu naufuta na atarekodi Aisha mtamu upya kabisa!, na kuanzia sasa nyimbo alizoimba Asia utamu akiwa na wakaliwao kama vile subira haina kikomo, Fungu la kukosa, Sioni thamani ya pendo na hii mpya najuta kupenda zitaimbwa nae Aisha mtamu. Yeye Asia utamu namruhusu aende bendi yoyote ile akaendeleze kipaji chake zaidi sina tatizo nae.alimaliza kusema mkurugenzi thabit abdul.

         Tazama ustadi wa uimbaji pamoja na sauti tamu toka kwa Aisha mtamu akiimba wimbo wa najuta kupenda alipokuwa mazoezini pale wakaliwao modern taradance jana mchana. Video hii ambayo nitaiweka  katika blog hii muda mchache ujao, itakufanya wewe kama mdau kumjua na kumtambua vyema muimbaji huyu mpya wa wakaliwao modern taradance!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni