TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 5 Desemba 2015

WAKALIWAO, MSAGASUMU NA DOGO JACK SIMELA KUFANYA YAO NDANI YA HIZZA HALL MAJOE KESHO JUMAPILI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Ile show bab-kubwa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na wakazi wa majoe bwela na vitongoji vyake, inayowahusu bendi ya wakaliwao, msagasumu na dogo jacky simela inatarajiwa kufanyika kesho jumapili tarehe 6/12/2015 katika ukumbi wa hizza hall kuanzia saa kumi jioni mpaka sita kamili za usiku.
WAKALIWAO-TEAM MASAUTI.

              Mkurugenzi wa bendi ya wakaliwao modern taradance thabit abdul amesema kuwa vijana wake wapo tayari kabisa kushusha burudani ya nguvu kwa wakazi wa majoe bwela na vitongoji vyake, unajua ndugu mwandishi hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa sisi wakaliwao kufanya show maeneo ya majoe hivyo tunawaahidi wapenzi na wadau wetu wa maeneo hayo watapata kitu roho inapenda.

MSAGASUMU.

     Msagasumu kwa upande wake alisema kuwa anaamini ana mashabiki wengi sana maeneo ya majoe hivyo amewataka wajitokeze kwa wingi kushuhudia ni kwa nini muheshimiwa lowasa alimkubali kwa kazi zake! washikaji zangu wa bodaboda na bajaji waje kwa wingi kupata radha live toka kwangu.

DOGO JACK SIMELA.

        Nae dogo jacky simela alisema kwamba anaamini wapenzi wa mnanda au mchiriku wapo wengi sana maeneo ya majoe, wamekuwa wakinisikia tu kazi zangu lakini sasa kesho wataniona live na kupata burudani, nyimbo zote za jagwa musica ambazo zimekuwa zikifanya vizuri nitazicheza pale hizza hall. Wapenzi, wadau na mashabiki mmeombwa kujitokeza kwa wingi hapo siku ya kesho jumapili,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni