TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 12 Februari 2016

ISSA KAMONGO AACHIA WIMBO MPYA "NO COMMENT" KAMA ZAWADI YA VALENTINE KWA MASHABIKI WAKE.

NA KAIS MUSSA KAIS.


               Muimbaji Issa kamongo leo ameachia wimbo wake mpya uitwao "No comment" na kusema kuwa wimbo huo ameamua kuuachia kipindi hiki ili uwe maalum kwa mashabiki zake katika kusherehekea siku ya wapendanao yaani valentine day.


ISSA KAMONGO.

           Wimbo huo ambao ameimbia katika bendi yake ya sasa supershine modern taarab ni mzuri sana na mara kwa mara umekuwa ukiombwa kurudiwa kuimbwa upya kila wanapopiga show zao, huu wimbo ni utunzi wangu mimi mwenyewe, kinanda amenipigia dogo shamte, solo bwigabwiga na gitaa la besi amepiga shabban madobe hii ni supershine original hakuna wa kuazima hapo kaka, alijigamba Issa kamongo. Nautoa kama zawadi kwa mashabiki wangu hususani kipindi hiki cha valentine kwani nawapenda sana na najua walikuwa wamenimiss sana maana tokea nimetoa wimbo wangu wa mwisho penzi la kimataifa ni muda mrefu sasa.


           Mtandao huu kama ilivyo ada tutauweka wimbo huo ili wadau na wapenzi wake wapate kuusikiliza na kudownload ili wapate kuburudika, hongera sana Issa kamongo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni