TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 27 Februari 2016

KAPTEN TEMBA ASHINDWA KUWATHIBITISHIA WATANGAZAJI MAHUSIANO YAKE NA BISHARA ADEN WA MOMBASA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


               Mkurugenzi wa fungakazi modern taarab na mtunzi wa mashairi kapten temba usiku wa jana aliwekwa "kikaangoni" katika group la whatsap la watangazaji wa taarab wa redio na televisheni tanzania liitwalo "ubuyu wa taarab" na kuulizwa maswali kwa muda wa masaa mawili.

KAPTEN TEMBA NA BISHARA ADEN KAMA WANAVYOONEKA KATIKA WHATSAP PROFILE.


           Aliefungua utaratibu wa maswali kwa mgeni huyo ambae aliwekwa kwenye sagment iitwayo "kikaangoni wiki hii" ni mtangazaji wa mbeya fm iliyopo mkoani mbeya Asha athuman ambae alimuuliza temba kuwa katika profile picture yake whatsap kaweka picha yake pamoja na ya Bishara aden mtangazaji wa pwani fm mombasa na kutupia status moja matata sana je wana mahusiano ya kimapenzi?.


        Temba alijibu kwa mafumbo kidogo na kusema " Bishara ni msichana mrembo, pia ataechomoza nikampenda ntaoa sababu sipendi kuzini" kwani mnapenda awe na mie?.


KAPTEN TEMBA KATIKA POZI.

    Aliefuatia kuuliza swali ni mtangazaji wa ebony fm ya mkoani iringa aitwae Tinna tunner nae aliuliza kama ifuatavyo Temba nasikia Bishara ana mchumba wake huko mombasa, sasa wewe dizaini kama umedandia penzi la watu na ndio maana Bishara hataki utangaze mapenzi yenu je ni kweli na kama ni kweli upo tayari kuwa kidumu maana mapenzi upofu!.


         Temba alijibu kuwa Bishara hana mchumba na wala hajawahi kuolewa msimzibie ridhiki, kuhusu bishara naona vichwa vyenu vinawauma sana kuniona nina shombe shombe eeeeh!!.


     Nae Diva mtangazaji wa hits fm zanzibar aliuliza kama ifuatavyo, katika bendi yako aliekuwa akijulikana sana ni Ashura machupa na Amina juma na kwa sasa mmoja amesepa hapo vipi mbona fungakazi ipo kimya? na vipi kuhusu wimbo wa khadija kopa "hakuna mwenye mji wake" watanzania wategemee nini kipya kutoka kwako?.


          Temba alijibu, kuhusu Ashura machupa wala sio pengo kwetu ni muimbaji wa kawaida sana, wapo wenzie kama yeye wengi. na huu wimbo mpya wa khadija kopa ni mzuri sana wadau wajiandae kuupokea, ngojea niwape mashairi yake kidogo..."mapenzi sio biashara mumeo ananilipa, kwa paundi na dollah hadhi ananipandisha, dilla ulovaa wewe la kutamba harusini, nachambulia mchele msibani na hitimani, dongo hili stret liendee sina wakumuhofiaa, mtaishia kunipiga vijembee na bwana kashaamuaa, mara huyo niliomchukulia bwanaa njiani tunasalimianaa".  Habari ndio hiyo!.


HII NI PROFILE PICTURE YA WHATSAP YA TEMBA KAMA INAVYOONEKANA KWA SASA!.

      Maria mtangazaji wa kwizera fm ngara nae alimuuliza temba kwamba kwanini ndoa nyingi za mastaa huwa hazidumu?


            Temba akajibu kwamba kuhusu kudumu kwa ndoa ni mipango ya mungu tu, mwayajua  yetu kwakuwa sisi ni kioo cha jamii na nyie watangazaji mna yenu ya kutungiwa filamu!.


         Watangazaji ni wengi sana waliomuuliza maswali kapten temba nae akawajibu labda niwataje kwa majina tu baadhi, kaka zema wa citizen redio, Najma amiry wa mwambao fm tanga, fortina mbawala wa CG FM ya tabora, Koleta makulwa wa redio free africa mwanza, malick wa hits fm zanzibar, pili nyenje au mama nyeupe, Edna wa Afm ya dodoma, Rachel wa pamoja fm mpanda, Rehema nyamaka wa redio one na wengineo. Ila wengi wa watangazaji hawakupata nafasi ya kushiriki kwa kuwa walikuwa katika vipindi vyao!. ila temba tutamrudisha tena siku zijazo maana watangazaji wengi walitaka kumuuliza ila walibanwa sana na kazi zao redioni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni