TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 25 Februari 2016

MISHI B! UKIPENDA MUITE "MISS TWIGA" NI NYOTA ING'AAYO NDANI YA JAHAZI MODERN TAARAB KWA SASA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

               Ukipata bahati ya kuhudhulia onyesho lolote la bendi ya jahazi modern taarab basi ni lazima utamuona msichana mrembo, mrefu mithili ya twiga, mwenye haiba ya kike na asiejua kununa, huyu si mwingine isipokuwa ni mwanahamisi mohamed au muite mishi B! Miss twiga asie na majivuno.


MISH B AKIIMBA STEJINI KWA KUJIAMINI MNO.

            Mtandao huu wa ubuyu wa taarab ulifanya mahojiano na muimbaji huyu chipukizi kwanza ukitaka kujua safari ya muziki ya mishi b, ni wapi alipitia mpaka kuingia jahazi modern taarab?, nae bila hiyana alikuwa na haya ya kusema. muziki huu wa taarab nimeanzia bendi moja iitwayo samsuri modern taarab, baada ya hapo nilijiunga na Ott bendi hii ni bendi ya chama cha mapinduzi ambayo ilikuwa ikisimamiwa na muheshimiwa Abbas mtemvu.

MWANAHAMISI MOHAMEDY "MISH B!".

                Lakini bendi yangu ya mwisho mpaka najiunga na jahazi modern taarab ni dealers modern taarab yenye maskani yake keko jijini dar, safari yangu ndani ya bendi ya jahazi ilikuwa kama ifuatavyo, kuna siku nilikwenda katika show ya jahazi nikakutana na mgeni kisoda  nikamwambia vipi kaka hivi ndani ya jahazi siwezi kupata nafasi nikajiunga nao?, yeye akaniambia jaribu bahati yako kamuone mfalme mzee yusuph pale alipokaa na umueleze hitaji lako! ndipo nilipokwenda na kuongea na mzee, yeye akaniambia anipe test pale niimbe malupelupe nikamwambia sawa, baadae kidogo nilitangazwa na kupanda steji na kuimba wimbo huo! nashukuru mungu niliimba vizuri sana! mzee akaniambia wao wanalalia safari ya mikoani na kesho yake wanasafiri kwahiyo kama nipo tayari naweza kuungana nao hivyo mimi bila kujivunga nilisafiri nao, na ndivyo ilivyokuwa na mpaka sasa nipo jahazi modern taarab.

HAPA AKIWA STEJI NA WASANII WENZAKE AMBAO HAWAONEKANI PICHANI.

           Katika muziki huu wa taarab msanii ambae namzimia kisawasawa ni sabaha salum muchacho kwa mwanamke na kwa mwanaume nampenda sana mfalme mzee yusuph kwa kazi zao nzuri za sanaa!. nawaomba wadau wa muziki huu wanipokee na wanipe sapoti kubwa ili nifikie malengo kama ambavyo wamefikia hadija omary kopa, mzee yusuph na malkia leyla rashid na wengineo alimalizia kusema.

MISH B AKIWA KWENYE POZI.

               Siku ya kesho mtandao huu tunaahidi kuweka wimbo wake mpya bibie huyu ambao ameimbia ndani ya jahazi modern taarab na ambao unafanya vizuri kupitia redio stesheni mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni