TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 10 Machi 2016

JAMALI MPERAMPERA:- NITAIFANYA ALJAZEERA MODERN TAARAB KUWA NI BENDI YA KUIGWA NA WADAU WOTE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MKURUGENZI WA ALJAZEERA JAMALI MPERAMPERA.

             Mkurugenzi wa aljazeera modern taarab Jamali mperampera  amejinasibu kuwa bendi yake kwa mwaka huu itakuwa ni bendi ya kuigwa kulingana na mikakati ambayo ameiweka yeye pamoja na mkurugenzi mwenzie Mohamedy salim almaarufu Dot Do!.


        Akizungumza kwa kujiamini katika club yao maeneo ya jangwani kariakoo Jamali alisema tumekuwa tukilisoma soko la muziki huu linataka nini kwa muda mrefu sana na ndio maana tumekaa na mwenzangu na kukusanya nguvu na kuja na ujio huu!, hii sio nguvu ya soda nawaambia wale wanaobeza, kuwa aljazeera hii sio ile ya zamani tutahakikisha wasanii na viongozi wa bendi hii wanapata kila hitaji ili kazi ibakie kuandaa vitu vizuri kwa ajili ya wadau na mashabiki wetu tu!.


         Kwa sasa tayari tumeachia nyimbo mbili mpya katika media mbalimbali na video zinakuja muda si mrefu ili hadhira itutambue ni kitu gani tumedhamilia kufanya kwa ajili ya soko la muziki huu wa taarab.Tumesha mchukua mpiga kinanda Hamisi chizi tokea gusagusa na bado tutaimalisha kikosi kulingana na mahitaji yetu, hakuna msanii ambae tutamtaka alafu tutamkosa hilo haliwezekani, kwani tumedhamilia kufanya makubwa zaidi safari hii alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyo Jamali mperampera.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni