TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 11 Machi 2016

KISOLO MWANA MALUI, KAMONGO MR BEAN NA SHABBAN WAKUMWAGA WAACHA KAZI DAR MODERN TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                Wanamuziki watatu wa bendi ya Dar modern taarab kisolo mwana malui, shabban wakumwaga  na kamongo mr bean wameachana na bendi hiyo na kila mmoja ameamua kujikita katika bendi ingine.

KISOLO MWANA MALUI AKIWAJIBIKA.


          Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa tatizo hili mpaka kufikia wao kuacha bendi kwa pamoja lilianzia siku ya wapendanao ambapo bendi yao hiyo ilikuwa ikifanya show ya pamoja na wakaliwao modern taradance na coast modern taarab pale maeneo ya temeke buliyaga bar. Wasanii hao wote kwa pamoja hawakutokea katika show hiyo jambo lililofanya dawati la habari la mtandao huu kuanza kuwatafuta na kutaka kujua toka kwao kulikoni mpaka wote kwa pamoja kutoonekana kazini siku hiyo?.


    KAMONGO:- Aaah! mimi kwa upande wangu nimechoka na ahadi zisizo kamilika kila kukicha, unajua bendi yetu haina zile show za mfululizo kwahiyo kiongozi mmoja aliniita na kuniambia nitafute biashara ya kufanya alafu niiende nikamwambie ili anipatie pesa ya mtaji ili nisiwe nategemea muziki tu! lakini tokea nimemfikishia taarifa za biashara ninayotaka kuifanya amekuwa kimya wala sijaona msaada wowote kwa upande wangu ila watu wengine wanasaidiwa hivyo nikaona labda mimi sio muhimu ndio maana nikaona ni bora niachane nao tu kwa amani.


 WAKUMWAGA:- Mimi kwa upande wangu pia kilichonifanya niache bendi ni tatizo la pesa pia, nimekuwa sithaminiki hata ninapotoa tatizo la aina yoyote sisaidiwi, alafu kinachouma zaidi kama kuna matabaka hivi kuna wanaosaidiwa zaidi na uongozi na akina sie ambao tunaonekana wa baadae, mimi siku hiyo ya wapendanao nilikuwepo sehemu ingine na bendi ingine nafanya kazi, sikuwa na sababu ya mimi kwenda huko dar modern wakati sina umuhimu wowote, nimeondoka na nipo nafanya show na bendi ingine sasa.


KAMONGO MR BEAN MPAPASA KINANDA.

  KISOLO:- Siku hiyo ya show yao ya wapendanao, mimi nilikuwepo tu nafanya mambo yangu mengine, kuna kiongozi mmoja alinipigia simu na kuniambia kuwa kuna show na bendi zingine mbili nami nikamjibu kuwa sikuwepo dar nilikuwa huko malui hivyo alinitumia nauli ya kurudi ili niwahii show lakini sikwenda kwa makusudi ndugu mwandishi!, kwa sasa nafanya zangu show na jahazi kolombwe kwa wiki mara tano sina wasiwasi na sihitaji tena kurudi huko dar modern, kikubwa nimekuwa nikifanywa wa baadae sana pindi ninapoeleza shida zangu kwa uongozi.


          Hayo ndio yaliyojili na kufanyiwa uchunguzi na mtandao huu, lakini pia tutafanya kila linalowezekana ili kuzungumza na uongozi wa bendi hii juu ya haya yanayozngumzwa na wasanii hawa ambao hawapo dar modern kwa sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni