TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 12 Machi 2016

YOUNG HASSAN ALLY:- NIMECHOKA KUTUMWA, SASA NAANDA MIN BEND YANGU MWENYEWE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                 Muimbaji wa ogopa kopa classic bendi Young hassan ally amefunguka na kusema kuwa amechoka kutumwa na kwa sasa anaanda cha kwake mwenyewe ili aendelee kulisongesha gurudumu.

YOUNG HASSAN ALLY.


         Akizungumza kwa kujiamini Hassan ally alisema kuwa haoni kama ni ngumu kumudu kwakuwa yeye ni mtunzi, muimbaji na hata fitna za muziki wa taarab anazijua maana yupo katika game hii muda mrefu sana!.


      Labda nichukue nafasi hii kuwaomba akina dada wote ambao wanajiona wana uwezo wa kuimba basi wanaweza kunicheki kwa namba zangu za simu ambazo ni 0719-893525 nahitaji wasichana wanaojua kuimba takriban wanne "4" ili tuanze kufanya kazi kwa pamoja, akizungumzia issue ya yeye kutolewa u-director pale ogopa kopa na malkia wa mipasho nchini khadija omary kopa, Hassan alisema kuwa hana tatizo na maamuzi hayo anayaheshimu na ataendelea kufanya kazi ogopa kopa bila tatizo lolote sababu anamchukulia khadija kopa ni sawa sawa na mama yake mzazi maana anamuheshimu sana.


         Ikumbukwe kuwa mtandao huu uliwahi kuandika habari ambayo ilikuwa inamuhusu yeye hassan ally kushushwa na kuwa msanii wa kawaida ndani ya bendi ya ogopa kopa na mkurugenzi khadija omary kopa, kwa sasa bendi haina director baada ya hassan kuondolewa katika nafasi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni