TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 10 Machi 2016

WADAU NA MASHABIKI WA TEAM OGOPA KOPA KUKUTANA JUMAPILI TAREHE 13/03/2016 MAGOMENI MWEMBECHAI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


           Wadau na mashabiki wa team ogopa kopa classic wanatarajia kukutana katika kikao chao cha kujadili mambo kadhaa wa kadhaa ukiwemo uzinduzi wa bendi na albam ya bendi hiyo.


          Akizungumza na mtandao huu mratibu wa kikao hicho black kopa alisema kuwa wale wote ambao wana mapenzi ya dhati na bendi yetu pamoja na malkia wa mipasho tanzania khadija omary kopa wanakaribishwa wafike kwa wingi tu, hata kama mpaka sasa hujajiunga na team ogopa kopa lakini unaipenda bendi basi unakaribishwa sana siku hiyo.


          Alitoa namba za simu kwa yeyote ambae atahitaji maelekezo zaidi ni namna gani anaweza kufika katika kikao hicho kwa maelekezo, basi anaweza kupiga namba hizi 0654-795973 atakutana na kijana aitwae Ibra! huyu atamuelekeza vyema. Mtandao huu unawaahidi wadau hao kuwa utatuma mwandishi wake katika kikao hicho na kuleta mrejesho hapa katika hadhara ya wasomaji wake ni nini kilichojadiliwa kwa maendeleo ya ogopa kopa na team nzima kwa ujumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni