TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 8 Machi 2016

WATANGAZAJI WAMUWEKA KIKAANGONI ALLY J KWA MASWALI NA MALALAMIKO MWENYEWE AWAOMBA MSAMAHA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

ALLY J MKURUGENZI WA FIVE STARS MODERN TAARAB.

                Group la whatsap "ubuyu wa taarab" ambalo ni maalum kwa watangazaji wa taarab afrika mashariki na kati, siku ya jana jumatatu kulikuwa na segment iitwayo "kikaangoni wiki hii" ambapo msanii mwalikwa alikuwa ni mkurugenzi wa five stars modern taarab Ally J.

           Hii ni segment ambayo msanii huwekwa kati na kushambuliwa kwa maswali mbalimbali toka kwa watangazaji tofauti toka tanzania na hata nje ya tanzania, na kwa siku ya jana kitimtim kiliwaka kweli na ilikuwa kama ifuatavyo twende kwa pamoja:-

 

  MWAJUMA RAS FM DODOMA:- Ally J karibu sana, swali langu kwako ni kwamba upo kimya sana je tuitegemee lini tena uwanjani five stars? na je mpaka sasa ni wasanii wangapi ambao wametoka katika bendi yako?.

 

   ALLY J:- Ukimya wa five stars ni mitihani tu ndio ambayo inatokea kwa binadamu, na kila siku nimekuwa nikihangaikia suala la vyombo na vikipatikana nina imani tutarudi upya tena na muda mchache ujao nina uhakika nitapata vyombo vyangu, wasanii waliohama bendi ni salha wa hammer Q na mariam B.s.s., zena mohamedy na mwamvita shaibu.

 

MALICK HITS FM ZNZ:- Ally J vipi kuhusu dua ya kuwaombea marehemu waliotangulia ambao walipata ajali wakati ninyi five stars mnaenda kufanya show mikoani, maana mara hii naona mpo kimya sana kaka kulikoni hapo?.

 

 ALLY J:- Kuhusu dua lazima ifanyike, lakini pia ni lazima watangazaji muelewe kuwa ajali ilipatikana tarehe 21 ya mwezi wa 3 panapo majaliwa tarehe hiyo tutakuwa tumetimiza miaka mitano na dua tutaifanya pale pale msikiti wa mtoro kariakoo na media zote mtatangaziwa.

 

NADRAH DREAM'S FM MBEYA:- Ally J, mimi napenda kujua toka kwako wewe kama mkurugenzi wa five stars ni wasanii wangapi mpaka sasa unaweza kuthibitisha kuwa wamebaki katika bendi yako?

 

 ALLY J:- Nadrah ni hivi kwa hivi sasa nikizungumzia wasanii waliokuwepo haiwezi kuwa nzuri sana kwa sababu bendi inapokuwa imesimama kwa muda kwa matatizo ambayo yalitokea ili kuyaweka sawa, mara nyingi wasanii huwa wanakwenda katika bendi zingine kujitafutia ridhiki, wenyewe tunaita ndondo

 

 TINNER EBONY FM IRINGA:- Ally J natambua umeshooting nyimbo kama mbili sikosei kwa Bobo mautundu, lakini cha ajabu mpaka sasa hujazigomboa zipo mikononi mwa Bobo na muda umepita je unaweza kutupatia sababu kiongozi?.

 

 ALLY J:- Tinner nashukuru sana kwa swali lako na kwaniaba ya wengine naomba mnisikilize vizuri jibu langu, mimi sikutengeneza nyimbo mbili pale kwa Bobo nimetengeneza albam nzima lakini mkataba wetu wa kimaongezi baina ya mimi na Bobo umekwenda tofauti na vile ilivyokuwa kwahiyo na maanisha kuna mkataba tuliwekeana na Bobo ikiwemo kwenda kuuza zile nyimbo kwa muhindi na yeye achukuwe chake kama gharama, ila haikuwa kama tulivyopanga na ndio sababu mpaka leo nyimbo anazo yeye.

 

 PILI NYENJE UPLAND REDIO NJOMBE:- Mwanzoni ally j tulikuwa tukifanya kazi na wewe vizuri sana tu, lakini ikafikia wakati sijui ulikuwa na mawazo yako sijui kuna mtu alikukwaza, nilikupigia simu mimi na nikakuomba tufanye interview, lakini ulinijibu jeuri sana tena kwa maneno makali tena ya karaha haswa, tokea hapo nikafuta namba zako na nikasema sitocheza nyimbo za five stars katika kipindi changu ndivyo ilivyokuwa mpaka leo hii unaingizwa humu katika group letu, na nilisema sitokuuliza chochote nitaangalia tu wenzangu wanavyokuuliza ila admin amenilazimisha mimi kukuuliza na ndipo nikapanda hewani kama hivi, ally j wewe sio! ally j unadharau sana.

 

  ALLY J:- Mimi labda nianze tu kukujibu swali lako pili nyenje au mama nyeupe, kusema ukweli wa mungu mimi sinaga hiyo twabia ila kuna uwezekano pengine mimi binadamu aidha kweli umepiga simu nipo mazoezini nipo vipi! lakini issue ya mimi kumdharau mtu wa media kusema kweli sina kabisa, ila mpaka umeongea hivyo inawezekana imetokea naomba nichukue nafasi kukuomba radhi samahani sana tena sana mama angu, mimi ni mwanao nivumilie.

 

               Maswali yalikuwa mengi sana toka kwa watangazaji mbalimbali labda ningewataja kwa majina baadhi yao ambao ni kaka zema toka citizen redio ya nairobi kenya, Hotie wa generation fm mbeya, Edna wa AFM dodoma, Rachel wa pamoja fm mpanda, sauda mkalokota wa zenji fm zanzibar, mc chinga wa dodoma fm, Bobo mautundu wa mlimani redio dar, Fetty wa kituro fm makete, na wengineo wengi sana! kumbuka kipengele hiki huwekwa hewani kila jumatatu kwa kuwaalika wasanii tofauti tofauti kuingia kikaangoni!.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni