TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 7 Machi 2016

MPIGA KINANDA HAMISI CHIZI AITOSA GUSAGUSA MIN BENDI NA KUJIUNGA NA ALJAZEERA BENDI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                     Aliekuwa mpiga kinanda wa kutegemewa wa bendi ya gusagusa min bendi Hamisi ally ramadhan almaarufu "Hamisi chizi" ameitosa bendi hiyo na kuamua kujiunga na aljazeera bendi, zote za magomeni jijini dar es salaam.

HAMISI CHIZI AKIWA STUDIO ZA SOUNDCRAFTERS TEMEKE JIJINI DAR.

                 Akizungumza na mtandao huu Hamisi chizi alisema kuwa amekuwa akivumilia mambo mengi sana ya manyanyaso toka kwa viongozi wa bendi ya gusagusa, wamekuwa hawaoni thamani yangu, dharau zimekuwa nyingi sana wanaweza hata wakakutukana hata mbele ya mashabiki, sasa hali kama hii inanishushia heshima yangu mimi kama msanii na siwezi kuvumilia.

         Kwanza kwanini unidharau? wakati mwanzoni nakuja kutokea unguja walikuwa wakininyenyekea na kunipa heshima zote lakini leo hii nimekuwa sina thamani tena...kwa kipi haswa? nimeamua kuwaachia bendi yao na mimi nimejiunga na aljazeera na kwa sasa tupo studio kwa Enrico kule temeke tunarekodi nyimbo mpya. Yaani ndugu yangu hawa jamaa wa gusagusa ilifikia kipindi wakakiuka kabisa makubaliano yetu, maana umeme pale ninapoishi tulielewana wawe wananilipia lakini siku zingine nilikuwa nalala na kiza kulipa tena wakawa hawalipi.

         Mimi nawaambia waendelee wasiwe na presha kwani kwa sasa nipo huku aljazeera na mahitaji yangu ya ulazima napata kama kawaida sina tatizo alisema Hamisi chizi. Ikumbukwe kuwa bendi hizi zote zinapiga ile miondoko ya "old is gold" taarab na wanapatikana magomeni jijini dar es salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni