TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 6 Machi 2016

MWAJUMA WA RAS FM DODOMA AWEKA WAZI PENZI LAKE NA BLACK KOPA, AWAONYA WALE WANAOMNYEMELEA!.


NA KAIS MUSSA KAIS.

              Mtangazaji wa ras fm redio ya dodoma mwajuma isumail au kama wengi wanavyopenda kumuita kichuna toka mkoani morogoro leo kwa kujiamini kabisa amefunguka na kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi na mtoto wa malkia wa taarab nchini khadija omary kopa aitwae "black kopa" na kusema anampenda sana!.

BLACK KOPA AKIWA NA MWAJUMA ISMAIL AMBAE NI MPENZI WAKE KWA SASA.

             Akizungumza na mtandao huu baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari hizi kuwa kuna tetesi zimezagaa kwa wadau na mashabiki wa taarab nchini kuwa yeye anatoka kimapenzi na black kopa je ni kweli taarifa hizi?, mwajuma alianza kwa kucheka na kuitikia kwamba ni kweli taarifa hizo, akiendelea kulithibitisha hilo alisema, mapenzi yangu na black kopa sio kificho tena kwani mpaka familia yake black kopa wananijua na dada zake huwa wananiita wifi yao!, mama khadija omary kopa pia ananitambua kwahiyo sioni sababu ya kuficha mahusiano yetu, nampenda sana black kopa na sina mwanaume mwingine zaidi yake.

KIUKWELI WAMEPENDEZA SANA!.

           Hivi karibuni nimepanga kuchukuwa likizo kazini alafu nimpeleke mchumba angu kwetu nikamtambulishe rasmi, ila mama yangu mzazi tayari nimeshamdokeza juu ya mahusiano yangu na black kopa na hana tatizo kikubwa mama yangu anapenda mimi niolewe na mwanaume wa kiislam, akizungumzia athari za umaarufu wao sababu mwajuma ni mtangazaji na black kopa ni muimbaji yeye alisema kikubwa ni kuaminiana maana kila mmoja anakutana na vishawishi toka kwa baadhi ya watu ila kubwa ni kujitambua upo na nani katika mahusiano na sio kuchanganya kwani hiki kipindi ni kigumu sana maradhi mengi mno, namuamini sana mchumba angu black kopa kamwe hawezi kunisaliti maana ni mtu anaejitambua, nami namhakikishia kuwa nampenda sana na wala siwezi kumsaliti alimaliza kwa kusema, nawaasa wale wote wanaomnyelea mpenzi wangu wakome kabisa, waangalie kwengine wasituharibie penzi letu wenyewe tunapendana kwa dhati!.

          Mwandishi wa habari hizi alinyanyua simu na kumpigia black kopa ili nae kwa upande wake azungumze juu ya mahusiano yao lakini hakupatikana hewani kwani alikuwa njiani kurudi dar maana siku moja iliyopita ogopa kopa walikuwa wanapiga show mkoani dodoma, ila tunawaahidi kuwaletea mahojiano na black kopa siku chache zijazo ili nae aseme mapenzi yake kwa mwajuma mtangazaji wa ras fm dodoma yapo kwa asilimia ngapi?.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni