TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 4 Machi 2016

VIONGOZI WA TAARAB NCHINI TOENI VIBANZI MACHONI, KWANINI MNALALA MCHANA WA JUA KALI?.


NA KAIS MUSSA KAIS.

                   Wasomaji wa ubuyu wa taarab karibuni sana katika kile kipengele chetu cha makala ya wiki na ningependa kuchukuwa nafasi hii kuwaomba radhi kwani kipengele hiki kimekuwa kikisuasua ila maboresho zaidi yanaendelea kufanyika ili mpate kitu kizuri zaidi.

               Siku ya leo napenda kuzungumzia viongozi wa bendi za taarab kujisahau na kushindwa kutangaza bendi zao ni wapi zinafanya show katikati ya wiki au mwishoni mwa wiki, zamani wakati nakuwa nilikuwa nikisikia bendi za dansi zikitoa ratiba yao ya wiki ni wapi wanapiga ili wadau na wapenzi wao wasipate tabu ya kujua wapi waifuate burudani, mpaka sasa fm academia na twanga pepeta bado zinao utaratibu huo.

            Utamaduni huu kwa upande wa bendi za taarab haupo kabisa pamoja na kwamba karibia redio zote hapa nchini zina vipindi vya taarab, kwakweli hii inashangaza sana, siku zote biashara ni matangazo sasa usipojitangaza ni nani atafahamu bendi yako inapiga wapi? hivi ukiiambulia kupata wahudhuliaji wachache katika show yako utamlaumu nani? hayo makampuni makubwa kama coca cola, serengeti na hata sigara kila kukicha wamekuwa wakibuni matangazo mapya na kupeleka redio nia na madhumuni ni kutangaza bidhaa zao wanazozizalisha ili waendelee kupata wateja zaidi.

           Kwanini mnajiweka nyuma nyuma na kuufanya muziki huu wa taarab kukosa hamasa iliyozoeleka?, mtandao wa ubuyu wa taarab ni moja ya sehemu ambayo mnaweza kupitisha matangazo yenu na yakasomwa na wadau wengi sana, kuna redio mbalimbali, televisheni na hata magazeti tumieni fursa hizi basi katika kuutangaza muziki wetu wa taarab, dawati la habari la ubuyu wa taarab tunafungua milango kwa bendi zote za taarab nchini kutuma matangazo yao ya show kwa njia ya email ambayo ni mussakais@gmail.com au unaweza kupiga simu 0657-036328 au unaweza kutuma tangazo lako kwa whatsap kwa namba hiyo hiyo na litafanyiwa kazi! mtandao huu haufungamani na bendi yoyote ile na tunaahidi bendi zote zitapewa kipaumbele bila kujari ukubwa au udogo wa bendi husika.

            Mwisho kabisa tunapenda kuwaasa viongozi wa taarab nchini kuwa na tabia ya kukutana japo mara moja kwa mwezi na kujadiliana malengo na mikakati yao katika kufanikisha muziki huu unasonga mbele zaidi...Alamsiki tuonane wiki ijayo!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni