TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 9 Machi 2016

MKURUGENZI:- ALJAZEERA MODERN TAARAB TUMEDHAMILIA KUFANYA MAMBO MAKUBWA MWAKA 2016/2017.

NA KAIS MUSSA KAIS.

MKURUGENZI WA ALJAZEERA MODERN TAARAB-MOHAMEDY SALIM- DOT DO!

             Bendi ya aljazeera modern taarab yenye maskani yake kariakoo mtaa wa kongo na nyati, kwa sasa imekuwa ikisuka kikosi chake na kuandaa nyimbo zao mpya zipatazo nne kali zaidi.

 

          Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi mkuu wa bendi hiyo mohamedy salim almaarufu "Dot do" alisema kuwa safari hii tumerudi kivingine kwani tunatengeneza nyimbo zetu wenyewe na mpaka sasa nyimbo 2 tayari tumesharekodi, nimeongeza kikosi changu kwa kumuongeza Hamisi ally ramadhan au almaarufu Hamisi chizi huyu ni mpiga kinanda ambae alikuwa bendi ya gusagusa ya jijini dar es salaam., vile vile wapo waimbaji wapya ambao nimewaongeza ambao ni Ummi hamisi, salma sambwanda, mzee maneno  na fatma milulu.

 

       Nimepanga kuifanyia mambo makubwa sana bendi yangu nikishirikiana na mkurugenzi mwenzangu Jamali mperampera na viongozi wengine waandamizi, unajua kaka mimi shughuli hizi za muziki sijaanza leo ndugu yangu, ni muda mrefu sana na kuna baadhi ya vikundi nimevisaidia kwahiyo muda huu nimeelekeza nguvu katika aljazeera modern taarab. mipango yetu ya kimaendeleo naamini itafanikiwa na tutafika mbali kwa uwezo wa mungu.

 

      Mwisho kabisa nawaomba wapenzi na wadau watupokee na wazisikilize kazi zetu na kutoa maoni yao juu ya ubora wa nyimbo hizo. Baada ya kumaliza kurekodi nyimbo zingine 2 ambazo nazo zipo tayari tunatarajia kufanya video kabisa ili wadau waitambue aljazeera modern taarab. ikumbukwe kuwa bendi hii ya aljazeera wanapiga style zote za taarab nikiwa na maana kuwa old is gold pamoja na modern ndio maana bendi inaitwa aljazeera modern taarab alimaliza kwa kusema.

        

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni