TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 9 Machi 2016

FATMA MILULU:- TULIFUKUZWA DAR MODERN KWA UONEVU, ILA KWA SASA NATESA ALJAZEERA MODERN TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Muimbaji Fatma milulu ambae hapo awali alikuwa katika bendi ya Dar modern taarab, kwa sasa yupo ndani ya bendi ya aljazeera yenye maskani yake mtaa wa kongo na nyati jijini dar.

MUIMBAJI WA ALJAZEERA FATMA MILULU.


         Akizungumza na mtandao huu katika club ya aljazeera, fatma alisema kwamba kamwe hatoisahau siku ambayo walifukuzwa katika bendi ya Dar modern, tena kwa uonevu wa dhahiri kabisa, sababu makosa ya mwenzetu yalikuwa ya wazi na sote waimbaji tuliamua kushuka stejini na kumuachia yeye aimbe, unajua ilikuwaje ndugu mwandishi!, tulifanya ziara ya mikoa ya nyanda za juu kusini mikoa ya iringa mpaka mbeya.


      Katika show zote tulizifanya kwenye mazingira magumu mno ila tulivumilia, sasa wakati tupo katika show ya mwisho nahisi kama ilikuwa mbalali ndipo huyu mwenzetu akaja tena katika private car na bosi, sisi tukapanga kwamba kama ataimba basi tushuke kwa pamoja kuashiria kwamba hatukulidhika na kilichokuwa kinafanyika na ndivyo ilivyokuwa.


      Tuliporudi dar tukafukuzwa wasanii takribani 13 nikiwemo na mimi, lakini siku zote waswahili wanasema kuwa ukimpiga teke chura ni sawasawa na kumuongezea mwendo tu, na ridhiki kama ipo basi ipo tu kaka angu, kwa sasa nipo zangu aljazeera na tayari nimerekodi wimbo mpya na hivi karibuni utaanza kuchezwa katika media mbalimbali alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni