TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 14 Aprili 2016

AMIN SALMIN AKILI KUWA JAHAZI MODERN TAARAB IPO JUU KWA UBORA KWA SASA, AKANA KUWA NA BIFU NA MZEE YUSUPH.

NA KAIS MUSSA KAIS.

AMIN SALMIN AKIWA NA MKEWE JOKHA KASSIM.

           Mkurugenzi wa Tanzania motto modern taarab "t motto" Amin salmin amesema hana bifu wala ugomvi wowote na mkurugenzi wa jahazi modern taarab mzee yusuph.

 

     Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na watangazaji katika kile kipengele cha "kikaangoni wiki hii" baada ya kukutana na swali hilo toka kwa mmoja wa watangazaji hao, yafuatayo ni baadhi ya maswali na majibu toka katika group la watangazaji wa taarab whatsap lijulikanalo kama ubuyu wa taarab.

 

MWAJUMA RAS FM DODOMA:- Ni kwanini Amin salmin huwezi kutunga wimbo bila kumjibu mzee yusuph, hasa hasa nyimbo za mkeo jokha kassim asilimia kubwa bila kupepesa macho zinamlenga leyla rashid.

 

 AMIN SALMIN:- Ni kweli kama usemavyo kuna upinzani wa kibiashara upo baina ya mimi na mzee lakini ni upinzani wa kikazi zaidi, alafu mimi simjibu mzee yusuph najibu shairi, na ninavyofanya vile naonyesha ubora wangu katika kutunga na wala sivinginevyo!.

 

DIVA WA HITS FM ZANZIBAR:- Salm alaykum kwanza ningependa kujua toka kwako hiki kimya cha t motto kwa muda mrefu kinatokana na nini? pia huoni kama siasa inakupoteza kwenye muziki?.

 

AMIN SALMIN:- Suala la t motto ipo, isipokuwa ni mimi mwenyewe ndio nilikuwa na matatizo ya kiafya tu, na swali lako la pili ni kwamba siasa haiwezi kunipoteza mimi katika muziki, hii ilikuwa ni kazi maalum kwa ajili ya uchaguzi tu na sasa umeisha hivyo najipanga kurudi dar es salaam kuendelea na mapambano ya kuisimamisha taarab na t motto kwa ujumla.

 

SALMA MASHALLAH WA MAISHA FM DOM:- Katika tasnia hii ya taarab ni mafanikio gani makubwa ambayo umeyapata ya kujivunia?, na unapotunga nyimbo za kumjibu msanii fulani hudhani kuwa unaweza kupoteza fans wako watakaodhani kuwa unapenda shari?.

 

AMIN SALMIN:- Kwanza nijibu swali la kwanza, kwakweli tokea nimeunda bendi ya t motto imekuwa haijasimama kwa muda mrefu kwahiyo ni ngumu kusema nilipata mafanikio zaidi ya kutoa albam mbili tu, swali lako la pili nakujibu kama ifuatavyo, kwanza naomba ufahamu kuwa taarab ni majibizano mfano ni kwa hadija kopa na marehemu nasma khamisi kidogo, mimi sioni kuwa napoteza mashabiki isipokuwa nimekuwa nikijiongezea mashabiki kwa nyimbo zangu ambazo nimekuwa nikizitunga.

 

GRACE SINYORITA SAUTI FM MWANZA:- Kuna tetesi kuwa nyie kama t motto kuna wimbo mpya mnauandaa kuwajibu jahazi modern taarab, je ni wimbo upi? pia unaonekana unayo hofu kubwa na jahazi ndio maana ulishawahi kuwachukuwa wapiga vyombo wake mfano jumanne ulaya, unafikili hofu yako ni nini kwa jahazi modern taarab?.

 

AMIN SALMIN:- Si kweli kwamba tunaanda nyimbo kwa kuijibu jahazi modern taarab isipokuwa tunamjibu mshairi, ni kweli kuna wimbo tunataka kuurekodi unaitwa hakuna kuomba poo, na kusema kwanini tumekuwa tukiijibu jahazi tuu, lazima tukubali kuwa jahazi kwa sasa ndio bendi ambayo ipo juu sasa huwezi kufanya ushindani na bendi ambayo ipo chini isipokuwa ni lazima utatafuta bendi ambayo ipo juu ndio ushindane nayo.

 

SHUFAA WA KAYA FM BAGAMOYO:- T motto mmetoweka kwa muda mrefu na sasa mnarejea je kuna ongezeko au upungufu wa wasanii kama wapiga vinanda, waimbaji na wengineo? na mpaka sasa mmeanda nyimbo ngapi na ni nani watakaoimba nyimbo hizo mpya?.

 

AMIN SALMIN:- Kwakweli kama unavyofahamu utaratibu wangu mara nyingi mimi hutafuta wale waliosomea muziki huu, na wapigaji wa vyombo wapo wakiongozwa na omary kisila na upande wa waimbaji jokha kassim na katika albam hiyo kutakuwa na nyimbo tano ikiwemo hakuna kuomba poo na wimbo mwingine unaitwa mchawi ndugu ambayo ataimba muimbaji mpya kabisa.

 

MAMAA MADIKODIKO PILIPILI FM MOMBASA:- Amin salmin mimi ngependa kujua bado upo na mkeo jokha kassim?.

 

AMIN SALMIN:- Mamaa madikodiko, bado nipo na mke wangu jokha kassim kama kawaida ndugu yangu tuende wapi.

 

           Kwakweli maswali yalikuwa mengi sana nikisema niyaorodheshe yote hapa naweza kujaza page nzima ila baadhi yao ambao sikuweka maswali yao hapa lakini waliuliza pia ni malick shakran wa hits fm zanzibar, sauda mkalokota wa zenji fm zanzibar, fetty wa kituro fm makete, Asha wa victoria fm musoma, edna agustino wa Afm dodoma,koleta makulwa wa redio free africa mwanza, ummy ameir wa swahiba fm zanzibar, nadya omary wa bomba fm, sharifa wa kaya fm bagamoyo, Asha athuman wa mbeya fm ya mkoani mbeya na wengineo wengi, tunapenda kuchukuwa fursa hii kumshukuru amin salmin lwa kukubali kujumuika na watangazaji wa group la ubuyu wa taarab na kushiriki kujibu maswali kwa ufasaha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni