TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 14 Aprili 2016

OGOPA KOPA KUFANYA UZINDUZI WA BENDI NA ALBUM MPYA TAREHE 7/O5/2016 DAR LIVE MBAGALA

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Bendi yako uipendayo ya ogopa kopa classic chini ya malkia wa mipasho nchini khadija omary kopa inatarajia kufanya uzinduzi wa nguvu siku ya jumamosi tarehe 7/05/2016 katika ukumbi wa dar live mbagala jijini dar.


       Akizungumza na mtandao huu bora wa taarab nchini tanzania, mkurugenzi huyo khadija kopa alisema kwamba wamejipanga vyema kuzikonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wao siku hiyo na watazindua bendi sambamba na album mpya, vijana wake wapo kambini kwa muda mrefu sasa wakifanya maandalizi ya uzinduzi huo mkubwa ambao haujapata kutokea nchini.


      Kamwe sitowaangusha kwani hata mimi mwenyewe malkia kuna style maalum ambayo nimepanga kuingia nayo siku hiyo surprise kwa wapenzi, na nitafanya kitu tofauti kabisa na walivyozoea katika zinduzi za bendi zingine, katika uzinduzi huo ogopa kopa hawatokuwa peke yao watasindikizwa na vijana wa yamoto bendi, jahazi modern taarab chini ya mfalme mzee yusuph, msagasumu kabali yao bila kusahau wakaliwao modern taarab chini ya mkombozi thabit abdul, mashabiki mnaombwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani burudani zote hizo utazipata kwa kiingilio cha shilingi 10,000/= tu mlangoni nyote mnakaribishwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni