TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 14 Aprili 2016

KHADIJA YUSUPH, KIKAANGONI MBELE YA WATANGAZAJI 95 WA TAARAB NCHINI SIKU YA JUMATATU IJAYO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

KHADIJA YUSUPH SAUTI YA CHIRIKU MUIMBAJI WA JAHAZI MODERN TAARAB.

 

             Khadija yusuph au sauti ya chiriku muimbaji wa bendi ya jahazi modern taarab ya jijini dar es salaam, siku ya jumatatu ijayo tarehe 18/04/2016 anatarajia kuwa katika kikaango mbele ya watangazaji 95 wa taarab tokea mikoa mbalimbali ya tanzania pamoja na nchi jirani ya kenya.

 

      Akithibitisha kuwepo katika kipengele hicho ambacho kimeendelea kujizolea umaarufu miongoni mwa wadau wa muziki huu, khadija yusuph alisema kwamba amekubali kuwepo humo kwenye hilo group la whatsap la watangazaji na ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa sana kwa watangazaji hao.

 

     Unajua ndugu mwandishi, hawa watangazaji wamekuwa wakitusaidia sana kuutangaza muziki wetu wa taarab ambao kwa sasa unaonekana kuinuka tena baada ya kufifia kipindi cha nyuma, mimi sina tatizo kikubwa tuombe uhai na uzima siku hiyo ifike na nitaungana nao mapema sana alimaliza kwa kusema.

 

      Ubuyu wa taarab whatsap ni group la watangazaji wa taarab tu! ambao wametapakaa pande zote za nchi yetu ya tanzania na nchi jirani ya kenya hususani nairobi na mombasa!, msanii atakapoingizwa humo kwa muda atakaa kwa saa moja hadi saa moja na nusu huku akijibu maswali ya watangazaji hao kwa njia ya "voice note" ili watangazaji waweze kuichukuwa sauti ya msanii huyo na kufanyia kipindi siku ya pili katika redio zao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni