TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 13 Aprili 2016

JAMALI MPERAMPERA KUIPELEKA ALJAZEERA MODERN TAARAB DUBAI KWA SHOW TATU.

NA KAIS MUSSA KAIS.

          Mkurugenzi wa bendi ya aljazeera modern taarab, Jamali mperampera leo amezungumza na mtandao huu na kusema kwamba yupo mbioni kuipeleka bendi yake Dubai kwa show zipatazo tatu.

 

JAMALI MPERAMPERA-MKURUGENZI WA ALJAZEERA.

     Akifafanua zaidi mkurugenzi huyo alisema kwamba kwa sasa anafanya mawasiliano na jamaa sambamba na ndugu zake waliopo huko ili aweze kupata kumbi nzuri ambazo hazitokuwa karibu karibu, nia ni kuwapa burudani adhimu kabisa wakazi wa huko maana wamekuwa wakiisikia tu aljazeera modern taarab kuwa ndio mabingwa wa "old is gold" kwa sasa hapa nchini tanzania.

 

     Hii ni moja ya mikakati yangu katika mwaka huu 2016 kwa bendi yangu na wasanii wangu kwa ujumla, nataka ndani ya mwaka huu basi tuweze kufanya show nje ya nchi takribani kumi ndio nafsi yangu itaridhika, uwezo wa kufanya hivyo tunao mimi na mkurugenzi mwenzangu Dot Do! na hatuoni sababu ya kushindwa kufanya hivyo kwani kwa sasa tuna kikosi bora kabisa na mipango ya kukiboresha zaidi kikosi chetu inaendelea.Suala la kwenda dubai naamini mpaka tarehe 28 au 29 mwezi huu tutakuwa tayari tumeshamalizana nao wenzetu waliopo huko na kubakia sisi kupanga siku ya kuondoka na tarehe za show hizo pamoja na kumbi husika alimalizia kwa kusema mkurugenzi huyo asiependa kuongea sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni