TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 13 Aprili 2016

KAPTEN TEMBA AMJIBU SENIOR BACHELOR KWA KUMNYONYOA NA KUMDOBOA HASWA...PATA SHAIRI KAMILI HAPA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


KAPTEN TEMBA MKURUGENZI WA FUNGAKAZI MODERN TAARAB.
       Baada ya jana mtandao huu kuweka shairi zima zima la bendi ya bongo stars modern taarab ambalo ni utunzi wake senior bachelor, leo hii mkurugenzi wa fungakazi modern taarab kapten temba nae ametuma shairi la kumjibu senior ndani ya ofisi zetu za ubuyu wa taarab.

    Akizungumza kwa njia ya simu temba alisema huyo senior bachelor anatafuta kiki kupitia jina langu ila namuonya kuwa mimi sio level yake atafute watoto wenzie ajibizane nao mimi sina muda mchafu, ila kwa kumuonyesha kuwa mimi naweza nimeamua kutumia verse zipatazo mbili tu! ili ahangaike nazo.

      Mashairi ya wimbo huo ni haya hapa na yanakwenda kama ifuatavyo:-


                               Umekwisha huna swaga,   bora ukauze kuni
                               Maisha yamekupiga,    umehamia ukweni
                               Kupenda kwako kuiga,  inakushinda sabuni
                               Pasport yangu kubwa ntafika hadi marekani,  ya mombasa yamnekupa shida
                               Kuropoka hauchoki,  dereva wa bodaboda
                               Sasa kauze samaki,  wewe mpakaa poda na kuvaa vitaiti
                               Yangu yatakupa shida,  nnayo ya uturuki
                                Kama mie changu ndoa,  mama yako tumuite nani?
                                Hakuwahi kuolewa,  na morogoro anaishi na bwana
                                Kazaa watoto saba,  na wote wa zinaa
                                Kwenu adabu hamna,  wala hamkulelewa
                                Shida kwenu ipo sana,  mtoto wa miaka kumi anaishi na bwana.



   VERSE 2:-            Kama wako katulia,   mbona hukuukuta usichana?
                                Wapo walokuanza,   twawajua kwa mapana
                                 Pia wanaendelea,  kama habari hauna
                                 Mimba uliyoilea,  nenda kajiulize sana
                                 Nna mengi ya kuongea,  mda mchafu sina
                                 Kama ndoa tulioana sisi,  maneno ya nini?
                                 Kuachana pia tumeachana sisi,  inakuhusu nini?
                                 Usiseme ya wenzako,  ya juu uloyaona
                                 Pia nasi tuna yako,  ya marefu na mapana.



             Habari ndio hiyo, kama ambavyo niliwaahidi kuwaletea part 2 ya hili timbwili na kweli leo nimetimiza, mimi na wewe hatujui kikubwa ambacho wana gombea kapten temba na senior bachelor, katika hali ya kawaida tu ni ngumu kuamini kwamba hawa upinzani wao upo katika muziki tu! kuna mambo makubwa sana yamefichika baina yao, sababu senior bachelor amemuoa dada wa kapten temba, sasa jiulize kama ni shemeji yake ni nini haswa wanachogombea wawili hawa?, vuta subira utayajua kupitia hapa mtandaoni, endelea kufuatilia kisa hiki.



                              

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni