SENIOR BACHELOR, MKURUGENZI WA BONGO STARS TAARAB. |
Lifuatalo ni shairi husika sambamba na jina la wimbo:-
"CHANGU NDOA".
INTRO:- Sitishwi na john cenna, yule mcheza mieleka
Popote nitakusema, mimi mzimu wa under teka
Mkole umeutaka, mwali kigego nema juu
Nenda kafate talaka, kwa askari wa miguu
Ungenyamaza ningekusitiri, ili usihaibike
Imekuponza yako jeuri, acha uchambike.
VERSE 1:- Leo nakusema wazi, ili watu wakuelewe
Andikeni paparazi, ameyataka mwenyewe
Tena sipotezi wakati, nikam-search kwenye internet
Yeye si mtu classic, nikam-google aka up to date
Ng'ambo stori zimevuja, mpaka amedai talaka
Mume hana soko unguja, anajiuza mombasa
Mwenzangu una mikosi, upati bwana wa maana
Wa tatu teja wa nne si ridhiki, bwana mwenye wake bwana.
CHORUS:- Sitaki kuulizwa, kivipi ana watoto
Wala sio miujiza, ushangai michael jackson amewaacha watoto
Pengine amepandikiza mbegu, au kuna mtu wameshea
Bibi eeh acha kisebusebu, nakusema wewe changu ndoa
VERSE 2:- Dume la lilia ndoa, kilingeni kwa mganga
Anataka kuolewa, nyota ipate kupanda
Changu ndoa unaficha siri, ili bwana asiaibike
Ila ndio yupo dhahiri, ana haiba ya kike
Leo nakucheza msondo, wala sikupi nafuu
Umeshaachwa rudi kwa kondo, yule teja aliekubuhu
Mwenzangu umezoea, kuolewa na kuachwa
Ndoa tatu zimekupotea, nakusema umeyataka.
Hilo ndilo shairi la changu ndoa linavyoishia, hii ni kama tamthilia ina muendelezo mkubwa sana, mtandao huu utamtafuta huyo aliezungumzwa humu kwani tuna mjua alafu nae atueleze ana ushauri gani juu ya mashairi haya? tuwe pamoja katika kufuatilia muendelezo wa habari hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni