TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 9 Aprili 2016

ALJAZEERA MODERN TAARAB JUMAMOSI YA LEO NDANI YA DDC KARIAKOO,WANAWAKE BUREE USIKOSE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


         Bendi yako pendwa ya aljazeera modern taarab leo jumamosi kama ilivyo kawaida yao watashusha burudani ya nguvu ndani ya ukumbi wao wa nyumbani D.D.C. kariakoo kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo.


     Akizungumza na mtandao huu Director wa bendi hiyo Abubakar mgeni alisema kwamba wamejipanga vyema kuwalidhisha wapenzi wa bendi hiyo kwani wamekuwa kambini kwa ajili ya mazoezi ya nyimbo mpya na za zamani kwa takribani mwezi mmoja sasa, kikosi cha aljazeera kwa sasa ni moto wa kuotea mbali kabisa kabisa tunawaomba wapenzi wajitokeze kwa wingi leo kuja kupata raha na wala sio karaha kama za kule!.


    Nao wakurugenzi wa bendi hiyo Jamali mperampera na Dot do walisema kwamba wameamua kufanya wanawake bure ili kuwapa motisha zaidi kwani huu ni wakati wa wao kuja kwa wingi kupata burudani tokea hapa aljazeera modern taarab, pia kwa wale wanaotumia shisha tumeweka kuwa ni bure kabisa kabisa wataenjoy, nia ya aljazeera modern taarab ni kuwapa utofauti wa burudani, tunawaomba wajitokeze kwa wingi kwani tumefanya kiingilio kwa wanaume ni shilingi 6000/= na wanawake ni bure kabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni