TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 8 Aprili 2016

BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU AMIN SALMIN KUWEKWA KIKAANGONI NA WATANGAZAJI JUMATATU IJAYO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

       Mkurugenzi wa tanzania motto modern taarab "t motto" Amin salmin komandoo, baada ya ukimya wa muda mrefu hatimae jumatatu ya tarehe 11/4/2016 saa moja kamili usiku atakuwa kikaangoni akijibu maswali ya watangazaji wa taarab waliopo katika group la whatsap liitwalo ubuyu wa taarab.

MKURUGENZI WA T MOTTO AMIN SALMIN KOMANDOO.

     Akizungumza na dawati la habari la mtandao huu wa ubuyu wa taarab kutokea zanzibar, mkurugenzi huyo alisema amefarijika kwa kuona watangazaji wamempendekeza yeye awepo kikaangoni siku hiyo ya jumatatu, nina mengi ambayo nataka watanzania wayajue kwahiyo kupitia kipengele hicho naamini itakuwa rahisi kwangu kufikisha ujumbe kwa walengwa wakiwemo wadau na mashabiki wa t motto.

    Kikaangoni wiki hii ni sagment inayopatikana ndani ya group la whatsap ambalo limewakutanisha watangazaji mbalimbali wa muziki wa taarab kutokea tanzania na nje ya mipaka ya tanzania, kinachofanyika ni kwa msanii kuingizwa ndani ya group hilo kwa muda, tayari kwa kuulizwa maswali ambayo yeye atatakiwa kuyajibu kwa njia ya "voice note" ili watangazaji hao waweze kufanyia vipindi vyao wanavyo viongoza, Huu ni ubunifu wa kais mussa kais, tunasubiri na wengine waige!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni