TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 6 Aprili 2016

MASHA RAJAB DOLE MUIMBAJI WA MAMBO'S MODERN TAARAB YA MOROGORO ANAE VUTIWA NA ISHA MASHAUZI.

Na pambe za taarab


MASHA RAJAB DOLE MUIMBAJI WA MAMBO'S MODERN TAARAB.

          Wiki hii niliweza kufanya ziara katika mkoa wa morogoro na kufanya interview na bendi mpya ya taarab iitwayo mambo's modern taarab yenye maskani yake maeneo ya kiwanja cha ndege mkoani humo.


     Hawa jamaa mpaka sasa wameshafanikiwa kurekodi albam nzima yenye nyimbo nne ambazo ni "domo zipu iliyoimbwa na mariam mambo, husda za walimwengu imeimbwa na fatma yusuph pamoja na masha rajab dole, huizimi nyota yangu iliyoimbwa tena na mariam mambo na ya mwisho ni fisadi watu iliyoimbwa na mkurugenzi wa bendi hiyo mr dudu".


     Kilichonivutia zaidi ni uchakalamu wa huyu muimbaji "masha rajabu dole" kama utapata bahati ya kukutana nae na kumshuhudia akiwa stejini naamini hata wewe utavutiwa nae, kwanza mcheshi lakini pamoja na uchanga wake katika tasnia hii ya taarab nchini lakini amekuwa ni mtu wa kujituma sana na kukubali kazi za wale waliomtangulia, huyo ndie masha rajab dole mtoto wa morogoro mji kasoro bahari.


    Anasema kwamba muziki wa taarab anaupenda sana na amekuwa akivutiwa sana na uimbaji wa Isha mashauzi pamoja na khadija omary kopa, anaendelea kujinasibu kwamba hii bendi ya mambo's modern taarab ndio bendi yake ya kwanza tokea aingie kwenye sanaa hii na anamshukuru mungu tayari amesharekodi wimbo mmoja ambao ameimba sambamba na muimbaji mwenzie aitwae fatma yusuph, nina ndoto ya kufika mbali zaidi katika fani hii ya taarab nchini na namuomba mungu aweze kunisimamia ndoto zangu zitimie.


     Anapokuwa katika steji muimbaji huyu anajituma sana na wadau na wapenzi wa muziki huo mkoani morogoro wanamfananisha na fatuma nyoro wa jahazi modern taarab kwa kulishambulia jukwaa kwa minenguo yenye kumfanya shabiki ashindwe kukaa katika kiti chake, mtandao huu unakuahidi kukuletea habari nyingi pamoja na kuweka nyimbo zao mpya mtandaoni ili mzisikilize na wapo tayari kupokea maoni yenu wadau nini wafanye ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni