TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 6 Aprili 2016

SAKINA LYOKA WA NG'ARING'ARI CLOUD'S TV, USO KWA USO NA ALJAZEERA MODERN TAARAB MAZOEZINI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


      Mtangazaji wa kipindi cha ng'aring'ari cloud's televisheni Sakina lyoka akiwa na timu nzima ya wahusika wa kipindi hicho walitia maguu katika club ya aljazeera modern taarab iliyopo kariakoo jijini dar maeneo ya jangwani jirani na club ya yanga na kukuta vijana wakifanya mazoezi kama ilivyo ada yao!.


     Nia kubwa ni kufanya nao interview kwani kwa sasa bendi hii imekuwa gumzo hapa jijini mpaka kupelekea watazamaji wa kipindi cha ng'aring'ari kumuomba sakina lyoka kufanya mahojiano na wasanii wa bendi hiyo, Sakina alifika club mida ya saa nane mchana na kukuta mazoezi yanaendelea na yamepamba moto haswa!.


     Alipoingia ndani muziki ulizimwa na Director wa bendi hiyo Abuu mgeni alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wageni hao! ndipo sakina lyoka baada ya salamu akawaeleza nia na madhumuni ya wao kuwepo pale, kwani watanzania wanataka kujua kutoka kwao aljazeera modern taarab ni nini kikubwa wanafanya mpaka kwa muda mchache wamekuwa gumzo hapa jijini, nini sakina alizungumza na wasanii hawa? basi usikose kuangalia kipindi cha ng'aring'ari ndani cloud's televisheni jumamosi kwani mtayajua mengi ya ndani na yale yaliyofichika, zifuatazo ni baadhi ya picha chache zilizopigwa katika mahojiano hayo

 

SAKINA LYOKA AKIWA NA FATMA MILULU.

UMMI KHAMISI KUSHOTO, SAKINA LYOKA KATIKATI NA FATMA MILULU KULIA.
SAKINA LYOKA AKIWA NA MUIMBAJI WA ALJAZEERA PILLI SAIDI.


SAKINA LYOKA AKIWA NA MUIMBAJI WA ALJAZEERA UMMI KHAMISI.

SAKINA LYOKA AKIWAELEKEZA JAMBO WAIMBAJI WA ALJAZEERA.
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni