TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 5 Aprili 2016

WAKALIWAO MODERN TARADANCE WATAMBULISHA NYIMBO MBILI MPYA KALI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


        Bendi yako ya wakaliwao modern taradance yenye makazi yake jijini dar es salaam tanzania, siku ya leo wametambulisha nyimbo zao mbili mpya kabisa kupitia mtandao huu.


THABIT ABDUL-MKOMBOZI.

       Akizungumza na dawati la ubuyu wa taarab kwa njia ya simu mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema kwamba nyimbo hizo ni mfululizo wa zile zitakazo kuwa katika albam yao mpya ambayo itatambulika kwa jina la "ukinuna uwe na sababu" wimbo ulioimbwa nae Aysher othman vuvuzela, alisema kuwa nyimbo hizi majina yake ni "najuta kukufahamu" ulioimbwa na Hashim saidi na wa pili ni "kusudi haina pole" ambao umeimbwa na Asia hassan mjusi.


      Aliendelea kuzungumza kwa kuwaomba wapenzi wa wakaliwao modern taradance na wadau waendelee kuiunga mkono bendi ya wakaliwao kwani dhamira ya kufanya vizuri wanayo sana, kikubwa ni ushirikiano ili kufikia malengo tuliyojiwekea alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni