Unapolitaja jina la Ally J katika tasnia hii ya taarab hapa nchini juwa wazi umetaja mtu muhimu sana tena nguli wa muziki huu tanzania, hivi unajua sababu iliyopelekea akaitwa Ally jeuli na wadau wa muziki huu?.
Ilikuwa ni siku ya jumatatu ya tarehe 30/05/2016 pale katika ukumbi wa ikweta grill mtoni kwa azizi ally jijini dar es salaam ndipo nilipokutana na Ally J akiwa ni mmoja wa waliohudhulia sherehe ya ndoa ya msanii wa coast modern taarab aitwae said mitutu ambae amemuoa binti aitwae zainab juma, pamoja na mambo mengi tuliyoongea lakini lililonifurahisha ni hili la yeye kupewa jina la Ally jeuli na wadau wa muziki huu.
Alianza kwa kusema kuwa unajua kais, mimi ally J, sio mtu wa kuburuzwa na wamiliki wa bendi mbalimbali za taarab hapa nchini watu wamenipa jina la ally jeuli sababu mimi sio mtu wa kuitikia tu kila ninaloambiwa na hawa wanaojiita wakurugenzi wa bendi, mimi huwa nakuwa na misimamo yangu ambayo nataka ifuatwe lakini kiongozi anapokwenda kinyume na kile tulichokubaliana ndipo linapopatikana jina la "jeuli".
Kwa mfano unaweza kukuta tupo katika bendi kwa pamoja tunatengeneza wimbo mpya lakini ajabu wimbo unapotoka utakuta katika albam inaandikwa mtunzi fulani, muziki kaweka fulani huku ukichunguza kwa undani utakuta muziki labda nimeweka mimi ally j na utunzi wala sio wa huyo aliejiandika hapo kwenye kava, lakini kwakuwa yeye ni mkurugenzi basi anatumia mabavu kuandika tu! mimi siwezi kukubali jambo kama hili na nimekuwa nikilumbana sana na wamiliki wa mabendi kipindi hiko cha nyuma enzi za kutumwa, hivi ukiandika muziki huu kuweka ally j labda itakuwa umeharibu au? alihoji ally j.
Hii ni moja ya sababu ya mimi kupewa jina hilo na viongozi pamoja na wadau wa muziki huu hapa nchini, issue ni misimamo yangu mikali tu wala sio kitu kingine, lakini hivi karibuni nitatoa tamko langu rasmi juu ya muziki wa taarab na mimi ally j alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyu wa five stars modern taarab.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni