WAIMBAJI WA JAHAZI MODERN TAARAB WAKIWA STEJINI. |
Bendi yako ya jahazi modern taarab ya jijini dar es salaam kupitia kwa mkurugenzi mipango wake hamisi boha, leo wametoa ratiba kamili ya show zao kwa nzima kuanzia jumatano ya leo.
Akizungumza na mtanao huu kiongozi huyo alisema kuwa utaratibu huu wa kutangaza show zao kila wiki itakuwa ni pamanent kupitia blog hii bora kabisa ya taarab kwa sasa hapa nchini tanzania, kwahiyo wapenzi wa bendi hii wasikose kufuatilia habari zao kupitia hapa, alizitaja show hizo na kumbi zake kuwa ni:-
1. Jumatano watakuwa ukumbi wa koyanga kiwalani.
2. Alhamisi watakuwa ukumbi wa macho kodo bagamoyo.
3. Ijumaa watakuwa ukumbi wa check point chanika
4. Jumamosi watakuwa dar live mbagala katika uzinduzi wa ogopa kopa.
5. Jumapili watakuwa katika ukumbi wao wa nyumbani travetine magomeni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni