Bendi bora kwa taarab asilia kwa sasa hapa jijini dar es salaam, aljazeera wana mpera mpera hatimae wamefanikiwa kupata kiwanja kipya cha kukonga nyoyo za wapenzi wao kila ijumaa.
Akizungumza na mtandao huu, director mkuu wa bendi hiyo Abubakar mgeni alisema kwamba ni mapema sana kwa sasa kuanza kuitaja sehemu yenyewe sababu najua wafitini ni wengi sana wasio itakia mafanikio bendi yetu, unaweza kuitaja sehemu yenyewe alafu kesho na kesho kutwa unaambiwa usije kupiga tena hapa!. kwahiyo kwa sasa bendi itakuwa na show mbili, ijumaa itakuwa ni katika ukumbi ambao tutawatangazia baadae na show ya pili ni kama kawaida ndani ya ukumbi wa nyumbani D.D.C. kariakoo.
Akimalizia kueleza alisema kwamba anawashukuru wapenzi waliojitokeza kwa wingi sana katika show yao ambayo ilifanyika pale katika ukumbi wa D.D.C. kariakoo hivyo anawaomba kujitokeza kwa wingi kwani kuna kitu kizuri kimeandaliwa kwa ajili yako mashabiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni