TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 5 Mei 2016

JAHAZI MODERN TAARAB NDANI YA MACHO KODO BAGAMOYO ALHAMISI YA LEO...USIKOSE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MFALME MZEE YUSUPH NA MKEWE LEYLA RASHID WAKIFANYA YAO STEJINI.

         Bendi yako uipendayo ya jahazi modern taarab leo alhamisi wanatarajia kushusha burudani ya nguvu kwa wakazi wa bagamoyo na vitongoji vyake ndani ya ukumbi wa macho kodo bagamoyo kuanzia saa mbili usiku hadi majogoo.


         Bendi hiyo ambayo bado inaendelea na ile ziara yake ya kuwatangaza wasanii wake wapya Aisha othman vuvuzela na Zubeda mlamali imepania kuitikisa bagamoyo leo kwa show bab-kubwa ambayo haijapata kutokea, kiongozi wa bendi hiyo seif shiboli alisema kwamba kikosi chao kitafika mapema bagamoyo tayari kwa burudani hiyo, tunawaomba wapenzi waje kwa wingi kushuhudia burudani toka kwetu kwani siku zote sisi jahazi tupo makini na hatubahatishi.


       Hii ni nafasi pekee na ya kujivunia kwa wakazi wa bagamoyo hivyo mjitokeze kwa wingi kushuhudia jahazi modern taarab wakifanya yao ndani ya ukumbi huo wa macho kodo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni