TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 5 Mei 2016

ABDUL MISAMBANO:- SIO MIE NI MOYO NI WIMBO WANGU BORA ULIOSHEHENI UJUMBE MZITO WA MAPENZI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


ABDUL MISAMBANO AKIFANYA YAKE.

            Unapolitaja jina la Abdul misambano katika tasnia hii ya taarab hapa afrika mashariki, basi kila mmoja ataukumbuka wimbo wake bora uliotesa kwa miaka mingi zaidi kuliko nyimbo zote za kizazi hiki "ASU" ambao aliuimba akiwa na bendi ya babloom.


      Nilipata bahati ya kukutana na msanii huyu nguli katika viwanja vyake vya kujidai c.c.m. mwinyijuma mwananyamala yalipo makazi ya t.o.t. bendi na kupiga nae stori mbili tatu kuhusu muziki huu wa taarab nchini na mustakabari wake, kwanza nilitaka kujua ni nini siri ya yeye nyimbo zake karibia zote kufanya vizuri tofauti na msanii mwingine wa kiume hapa nchini?, nae alianza kwa kusema:- unajua ndugu mwandishi mara nyingi mimi huwa sikurupuki tu na kutengeneza nyimbo, siku zote nimekuwa nikisoma alama za nyakati na kuangalia soko letu linahitaji kitu gani muhimu kilichokosekana.


          Nyimbo zangu ukizichunguza sio za kukimbia kama hawa wanaotengeneza sasa hivi yaani "taradance", mimi nimekuwa nikitengeneza nyimbo za slow kidogo na zilizobeba ujumbe mzito wa kimapenzi, mimi nikizungumzia mapenzi huwa nazama ndani zaidi sio kama wengine na ndio sababu nimekuwa nikifanya vizuri mpaka sasa. watu wengi wanazungumzia mapenzi katika nyimbo zao lakini sio kama mimi, jaribu kusikiliza nyimbo zao alafu ulinganishe na zangu ndipo utaelewa ni nini namaanisha!. kuna huu wimbo wangu "sio mie ni moyo" huu ni wimbo uliosheheni ujumbe mzuri wa mapenzi na kamwe huwezi kuchoka kusikiliza, kwa kipindi hiki nasema ni wimbo bora wa kimapenzi wa karne ndugu mwandishi huo ndio ukweli halisi alisema misambano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni