TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 5 Mei 2016

MKURUGENZI WA ALJAZEERA TAARAB "OLD IS GOLD" DOT DO AREJEA NCHINI, NA JUMAMOSI HII KUWAONGOZA MASHABIKI UKUMBINI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

        Siku zote kitu kizuri huwa muelekeo wake unaonekana mapema na werevu wa mambo hukili wazi wazi kwamba hapa kazi ipo, hawa ni aljazeera modern taarab ambapo mkurugenzi wake Dot Do! amerejea jana jioni akitokea oman.

 

MKURUGENZI WA ALJAZEERA DOT DO AKIWA NDANI YA NDEGE.

       mkurugenzi huyo anatarajia kuwaongoza mashabiki lukuki ambao wamekuwa wakiongezeka kila kukicha katika ukumbi wa D.D.C. kariakoo jijini dar es salaaam tanzania. nimekuwa nikipambana kuhakikisha wasanii wangu wanakuwa na furaha wakati wote na ndio sababu hata ninapokwenda oman huwa sichelewi kurejea ili sote kwa pamoja tupeane mawazo ni nini cha kufanya ili kuwapa burudani mashabiki wetu, hivyo jumamosi hii nitakuwepo D.D.C. kariakoo sambamba na vijana wangu wa aljazeera, nawaomba wadau na wapenzi kuja kwa wingi ili kufurahisha nafsi zao kwa taarab asilia nzuri ambayo haichoshi.

 

        Bendi hii ya aljazeera modern taarab hufanya show zake ndani ya ukumbi huo wa D.D.C. kariakoo jijini dar es salaam na hupiga taarab asilia kwa wingi sana, hivyo mtandao huu unawaomba watu wajitokeze kwa wingi katika show hiyo mapema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni