KHADIJA YUSUPH-SAUTI YA CHIRIKU AKIWA KWENYE POZI.
Muimbaji khadija yusuph au ukipenda muite sauti ya chiriku ameuambia mtandao huu makini ubuyu wa taarab kwa njia ya simu kwamba hayupo tayari kuihama bendi yake ya jahazi modern taarab kama ambavyo imekuwa ikivumishwa na wadau pamoja na baadhi ya vyombo vya habari.
Khadija aliyasema hayo baada kusikia akizungumziwa sana juu ya yeye kuiacha bendi yake ya jahazi na kujiunga na bendi moja nguli ya taarab hapa nchini, napenda niwaambie wadau na wapenzi wangu kuwa mimi khadija yusuph au sauti ya chiriku sina muda wala mpango wa kuiacha bendi yangu kama inavyovumishwa!, mimi nashangaa sana watu wamekuwa wakinifuatilia sana sijui wanataka nini toka kwangu!, taarifa hizi zimekuwa zikinishushia heshima yangu sana na kuwafanya mashabiki wangu kupunguza imani na mimi.
Mtandao huu ulitaka kujua ni kwanini khadija yusuph hakusafiri na bendi ya jahazi modern taarab katika ile safari yao ya mikoa ya iringa, mbeya na songea ambayo jahazi wamerudi jana dar es salaam? na yeye alijibu kuwa sikusafiri na bendi sababu nilikuwa naumwa homa sana, na hao wanaovumisha kwamba nilikuwa na mipango ya kujiunga na bendi flani ndio maana nikabaki na si kweli kwamba nilikuwa naumwa nawaambia wataishia kuvumisha mambo yasiyo na uhakika mpaka mwisho wa uhai wao!, najua nia yao ni kunigombanisha na kaka yangu lakini nawaambia wameshindwa na wataendelea kushindwa milele, mimi nipo jahazi modern taarab na nitaendelea kuwepo hapo daima alimaliza kwa kusema khadija yusuph.
Mtandao huu umerekodi maongezi ya khadija yusuph wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ili iwe kama ushahidi siku ya siku!, na hii ni kwa nia njema tu maana huo ndio utaratibu wa mtandao huu wa ubuyu wa taarab.tunapenda kumpa pole khadija yusuph kwa tetesi hizi ambazo kwa namna moja ama ingine zitakuwa zimemuathiri kisaikorojia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni